Kwa kitaalamu fistula hujulikana kama njia isiyo ya kawaida inayounganisha mfuko wa mkojo na uke, ambayo huruhusu mkojo na/au haja kubwa kutoka bila kujizuia kwenye kuta za uke.
Nini hutokea?
Tatizo la kushindwa kujizuia kujikojolea na/au kupitisha haja kubwa kwenye tupu ya mwanamke linalojulikana kama fistula hutokea baada ya mwanamke kupata madhara kipindi cha kujifungua kutokana na kuwa kwenye uchungu wa kujifungua kwa muda mrefu (Prolonged and obstructed labor), kutokana na kichwa cha mtoto kushindwa kupita kwa urahisi kwenye tupu ya mwanamke.
Hali hii husababisha tishu za kwenye tupu ya mwanamke, kibofu cha mkojo na puru (rectum), kugandamizwa kati ya kichwa cha mtoto na nyonga za mwanamke. Hii husababisha mfumo wa damu kwenye tishu hizi kuharibika na tishu kukosa damu na kuwa katika hali inayojulikana kitaalamu kama ischemic necrosis. Baadaye tundu hutokea kati ya tupu ya mwanamke na kibofu cha mkojo au kati ya tupu ya mwanamke na puru.
Matokeo yake ni mwanamke kutoa mkojo na/au haja kubwa bila kujizuia kupitia tupu yake
Ukubwa wa tatizo
Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) linakadiria kuwa wasichana na wanawake wapatao millioni 4 duniani wanaishi na tatizo hili wakati kila mwaka wasichana na wanawake wengine 50,000 - 100,000 hupatwa na tatizo hili.
Fistula huonekana sana kwenye bara la Afrika na Asia ya kusini. Kwa Tanzania, wanawake na wasichana 1,200 kila mwaka hupatwa na tatizo hili. Katika tafiti mbili zilizofanyika Tanzania, iliripotiwa kuwa wanawake walio katika umri kati ya miaka 22-24 ndiyo hupatwa na tatizo hili zaidi.
VVF husababishwa na nini?
- Uchungu wa muda mrefu (Prolonged labour) ambao husababishwa na
- Kutokuwa na usawa wa uwiano wa nyonga ya mama na ukubwa wa mtoto (CPD)
- Mtoto kulala vibaya (malpresentation)
- Kutokuwa na usawa wa uwiano wa nyonga ya mama na ukubwa wa mtoto (CPD)
- Upasuaji wa kuondoa kizazi (hysterectomy)
- Upasuaji wa njia ya mkojo (repair of urethral diverticulum, electrocautery of bladder papilloma)
- Upasuaji wa kansa za nyonga (pelvic carcinomas).
Dalili
- Mkojo kutoka bila kujizuia kwenye kuba ya uke ndio dalili muhimu
- Kuna uwezekano wa kupata maambukizi hivyo dalili zifuatazo huweza kuambatana na dalili ya mwanzo homa na maumivu ya tumbo hasa ubavu na chini ya kitovu.
Vipimo
- Majimaji yanatoka kwenye kuta za uke huchunguzwa vitu vifuatavyo:
- Urea, creatinine, na potassium ili kuwa na uhakika kuwa ni VVF na sio Vaginitis (maambukizi ya uke)
- Mkojo huoteshwa kuangalia kama kuna vimelea na kujua dawa gani yaweza kuvimaliza vimelea hivyo
- Urea, creatinine, na potassium ili kuwa na uhakika kuwa ni VVF na sio Vaginitis (maambukizi ya uke)
- Rangi ya indigo carmine hutolewa kwa njia ya mshipa na pindi inapoonekana ukeni huthibitisha VVF
- Cystourethroscopy
- Intravenous urogram
Matibabu
Kama tatizo limegundulika siku chache baada ya upasuaji mpira wa kukojolea (urinary catheter either transurethral or suprapubic) huwekwa kwa siku 30. Fistula ndogo (chini ya sentimita 1) huweza kupona yenyewe au kupungua.
Upasuaji ili kurekebisha VVF, aina za upasuaji:
- V@#ginal approach
- Abdominal approach
- Electrocautery
- Fibrin glue
- Endoscopic closure using fibrin glue with or without adding bovine collagen
- Laparascopic approach
- Using interposition flaps or grafts
Baada ya upasuaji
- Mgonjwa huwekewa Suprapubic catheter (mpira wa mkojo) kwa siku 6 hadi 60 ili kupunguza mvutano wa nyuzi
- Vitamin C 500mg mara tatu kwa siku ili mkojo uwe wa asidi ili kuzuia maambukizi na kutengenezwa kwa mawe.
- Tiba ya kichochezi cha ostrogeni kwa wakina mama walikwisha acha kupata siku zao (postmenopausal)
- Dawa za kuzuia mshtuko wa mfuko wa mkojo-methylene blue na Atropine sulfate
- Antibaotiki
- Pumzisha nyonga kwa kuzuia tendo la ndoa kwa kipindi cha wiki 4 hadi 6. Ingawa wengine hushauri hadi miezi mitatu.
No comments:
Post a Comment