Sunday, March 18, 2012

Kulipa kisasi katika mapenzi ni kutengeneza kosa

Ninavyojua penzi la kweli lipo ndani ya moyo, lazima mtaoneana huruma na kutokuwa tayari kuipa uchungu mioyo yenu.
Ndani la penzi la kweli mtu huwa hatoki nje, huridhika na mwenzie kwa kuwa ndiye chaguo la moyo wake.

Mhusika katika uhusiano huo hayupo tayari kulipiza kisasi kwa kuwa anajua penzi la kweli halina kisasi bali kinachotakiwa kufanyika ni kumrudisha mwenzake kwenye mstari. Wapo wanaoshangaa kumwona mwanaume amemfumania mkewe na kumsamehe.

Mfano ukimfumania mkeo utachukua uamuzi gani? Nina imani asilimia 99.9 watasema: “Nitamuacha kwa kuwa si mwaminifu.”
Swali kama hilo ukiuliza kwa upande wa pili wa shilingi kuwa mkeo akikufuma wewe utachukua hatua gani? Hili sitaki jibu kwa kuwa unalo mwenyewe.

Kinamama siku zote huwa wanyonge, hata wakifumania huishia kulia tu.Nia yangu si kutaka mshindane kufumaniana, la hasha.
Hakika wengi wetu tumekuwa si waaminifu ndani ya nyumba. Kwa sasa imekuwa fasheni kila mtu kuwa na watu wawili nje au zaidi.
Ukiuliza utaambiwa kaanza mwenyewe au kanisingizia kwa muda mrefu, sasa ninafanya kweli. Huo ni uongo, kila afanyae kitu amedhamiria kwa muda mrefu, alitafuta sababu tu ya kufanya uchafu wake.

Kama si tabia yako, nakataa katu, kwani mtu kukusingizia haikupunguzii kitu mpaka uamue kulipa kwa kufanya kweli. Mwenzio asilie wivu, kisa utafanya kweli? Utatembea na wangapi kwa kusingiziwa? Au mpenzio kutembea nje?

Uchunguzi wangu ambao nina uhakika nao ni kwamba, asilimia 100, tabia za kulipizana kisasi kwa kutoka nje ya ndoa kwa kisingizio cha “unafanya kweli”, zinafanywa na wale ambao wamekuwa na asili ya tabia hiyo ila walificha makucha.

Hapa kuna mambo mawili. Kati ya watu wawili hao, kuna mmoja ambaye moyo wake hubadilika na kuwa tayari kuwa na wewe kwa shida na raha. Lakini mmoja huwa habadiliki, huu huwa mwanzo wa mateso ya mmoja.

Kwa kuwa ulikuwa hujauandaa moyo wako japo ulikubali kuwa na mwenzio, tatizo lolote linapotokea ni upesi kulipa kisasi, watu hawa siku zote hutaka mwende sawa, ukimzidi hakubali na yeye atalipiza ili muwe sawa.

Wajua nini hasara za kulipa kisasi cha mapenzi?

Tujiulize mapenzi ni nini?
Sote twajua mapenzi ni upendo wa dhati utokao moyoni mwa mtu.

YAMEKUJA KWA
SABABU GANI?

Si kwa sababu nyingine bali kuleta upendo, amani, kuondoa upweke na kuleta farijiko ndani ya mioyo yetu.

KISASI HAPA KINA NAFASI?

Jibu ni jepesi, hakina.
Wewe unayemfanyia kisasi mpenzio, je, una mapenzi naye?

Lazima utajibu huna mapenzi naye.

Hapo najua kutakuwa na sababu kibao kwa kusema kama wewe uliyelipa huna mapenzi, aliyeanza ana nini? Jibu ni lile lile, anayetoka nje ya maana halisi ya mapenzi hana mapenzi, si muanzaji au mmaliziaji.

KAMA MWENZIO AMETOKA NJE YA NDOA/UHUSIANO, UFANYEJE?

Jibu ni jepesi lakini linataka moyo. Kwa wengi, hasa wanaume, wapenzi wao wanapotoka nje ya ndoa, hufikiria kuachana nao.

Nafikiri kuzuia ni bora kuliko kutibu, kwani matibabu hugharimu zaidi. Ifikie hatua ya mtu kuridhika na mpenzi mmoja tu, wapo wanaosema ni vigumu.

Kwa hoja kwamba, kila kiumbe kimeumbwa kwa maumbile na mvuto wake.

Hapa ndiyo sehemu muhimu sana, kwenu wote mnaofuatilia hivyo, naomba ukimaliza kuisoma mwambie na mwenzio.

Lakini kona hii itawasaidia sana ambao ndiyo wanaanza, hata waliokwisha anza si vibaya kuelewa.

Siku zote macho yanapoona moyo hutamani, uwezo wa macho ni kuona vinavyoonekana siyo vilivyofichika kwa mwanadamu.

NINA MAANA GANI?

Huwezi kupenda bila kuona, japo wapo watu wa ajabu hupenda kwa sauti bila kujua mtu huyo yupo vipi, yeye akisikia sauti anamuumba mtu akilini mwake kumbe sivyo alivyo, ndiyo maana nimeongelea kile unachokiona.

Kupenda si kukurupuka, kumbuka kupenda siyo mwanzo wa ujana bali mwanzo wa familia iliyo bora. Hapa wengi huchanganya tofauti kati ya matamanio na kupenda.

MATAMANIO NA KUPENDA
Matamanio ni kutamani kitu ukionacho na moyo wako kuufanya mwili usisimke. Si kwenye mapenzi tu bali kwa vitu vingi.

Mfano, unatamani kuishi maisha mazuri lakini uwezo huna au unatamani kuvaa kama fulani, kwa vile uwezo unao, hapa lazima utanunua vile vitu kama fulani.

Tukija kwenye suala la kupenda, mwanzo wake huwa matamanio ambayo hujenga mazoea na kukirudia kile kitu akilini hata kama hakipo na kuwa tayari kuwa nacho.

Kwa upande wa mada yetu, huwezi kumpenda mtu kwa mara moja zaidi ya kumtamani.

Kumpenda mtu si kutaka kumjua ana nini ndani, bali kumpenda kama alivyo.

Lakini ukimtamani mtu, kuna kitu utakitegemea kama akili yako itakavyokutuma. Kwa mfano, kijana mtanashati lazima wengi hujua ana pesa au mambo yake safi, ukimpata mambo yako yatakuwa mazuri au umbile la msichana kwa matamanio yako utawaza kuna kitu fulani.

Katika watu kama hawa, wanapokosa kile walichokifikiria lazima mapenzi hupotea mioyoni mwao.

Watu kama hawa hawako tayari kukaa na mtu kwa muda mrefu, kwani hukinai kuwa na kitu kimoja muda mrefu.

Ila apendaye kama nilivyosema, haangalii una nini, yeye hukupenda kama ulivyo na siyo kakurupuka kukupenda, bali amekufuatilia kwa muda mrefu, huku akikujaza moyoni mwake. Lakini siku zote mtu kama huyu hucheza bahati nasibu, kuna kuliwa na kula.

No comments:

Post a Comment