Maneno aliyokuwa akiyatoa yule mwanamke yalinichoma sana. Nikabaini siri moja ambayo nahisi ipo kwa wanawake wengi walio kwenye ndoa na hata wale walio kwenye uhusiano wa kawaida kwamba, wanafikia hatua ya kutoa aina hiyo ya penzi eti ili wapenzi wao wasiwasaliti. Jamani hii inaingia akilini kweli?
Unafikia hatua ya kuhatarisha maisha yako kisa unataka kukamilisha ile sentesi ya kwamba unampa mumeo kila anachokitaka? Huo ni ulimbukeni na kama wapo wanaoendelea kufanya hivyo, wanajitafutia matatizo yatakayowafanya waje kujuta baadaye.
Ni kweli washauri wa masuala ya mapenzi wanaeleza kuwa, ili uweze kumshika vilivyo mpenzi wako unatakiwa kuhakikisha unampatiliza katika kila anachokitaka lakini hawakuzungumzia ishu ya wewe kukubali mapenzi kinyume na maumbile. Hawakurusu hilo kwa kuwa wanajua madhara ya kufanya hivyo. Sasa iweje leo ukubali kufanya dhambi hiyo eti kwa kuwa mpenzi wako kataka na unampenda?
Katika ulimwengu wa sasa wapo wanaume wa ajabu sana. Hawa ni wale ambao si wastaarabu. Wao hawaangalii madhara yanayoweza kuwapata wenzao bali wanaangalia kujifurahisha wao tu. Mbaya zaidi baadhi ya wanawake nao wamekuwa mbumbumbu.
Eti kwa kuogopa kuachwa au kusalitiwa wanasema bora wafanye hivyo. Jamani, ifike wakati tufikirie kila tunalolifanya katika maisha yetu ya kila siku. Zipo mbinu nyingi za kumridhisha mpenzi wako na wala asifikirie kukuacha wala kukusaliti bila hata kumkubalia afanye hivyo.
Pia unatakiwa kufahamu kwamba, unaweza kumpa mpenzi/mume wako mapenzi hayo lakini bado akakusaliti tu. Sasa kwa nini ujidhalilishe?
Ni kamchezo ka’ nyumba ndogo
Ukijaribu kuchunguza utabaini kuwa wanaoongoza kwa mchezo huo mchafu ni wale wezi wa mapenzi ambao hufahamika kwa jina la nyumba ndogo.
Hawa eti wanatumia mbinu hiyo kuwashika waume za watu. Kimsingi hii ni aibu na wanaokubali kufanyiwa hivyo wanajidhalilisha na hawawezi kudumu na wanaume wao.
Usithubutu kabisa
Mapenzi kinyume na maumbile licha ya kwamba yamekatazwa hata na vitabu vitakatifu, madhara yake kiafya pia ni makubwa. Wapo wengi ambao sasa wanajuta kwa kufanya mchezo huo kutokana na kupata matatizo wakati wa kujifungua lakini pia wengi wao imekuwa ni rahisi kuambukizwa magonjwa mbalimbali ya zinaa ukiwemo Ukimwi.
Ni laana
Wanaofanya hivyo wamelaaniwa na wanaweza kushangaa uhusiano wao unakumbwa na matatizo kisha kusambaratika kwani Mungu hawezi kuubariki ule unaokwenda kinyume na maagizo yake.
Ni suala tu la kukaa na kujiuliza, wewe mwanamke unapata raha gani kufanya mapenzi kwa njia ambayo haijaruhusiwa? Wakati mwingine nashindwa hata kuwaelewa hawa wanaofikia hatua ya kujisifia kuwa eti wanawaachia waume zao ‘wajisevie’ wanachotaka kwa kuwa wanawapenda.
Hivi watakuwa na akili timamu? Kumpenda mtu ndiyo uwe tayari kuhatarisha maisha yako kiasi hicho? Tena kwa taarifa yako wale wanaowakubalia wapenzi wao mapenzi kunyume na maumbile wanaonekana wajinga na wanadharaulika. Hakuna mwanaume anayeweza kumheshimu mwanamke anayeweza kuuweka rehani mwili wake kwa njia hiyo.
Nimalizie makala haya kwa kusema kuwa, kanuni ya kwamba unatakiwa kuhakikisha unampatia mpenzi wako kile anachokipenda inabaki palepale lakini umkubalie katika yake yasiyo na madhara kwako. Yale ambayo unaona yatakuletea matatizo, mkatalie kwa kumpa sababu za msingi. Kama ni muelewa atakuelewa, asipokuelewa kuwa tayari akuache lakini usihatarishe maisha yako.
No comments:
Post a Comment