Siku za hivi karibuni kumekuwa na mtindo wa watu kutoka na wake/waume za watu. Tatizo hili lipo zaidi kwa wanawake. Bila aibu huku akijua kuwa mwanaume aliyenaye ni mume wa mtu anatembea naye. Wengine wanatamba kwamba wao ni washindi.
Kwamba wake zao hawana lolote, ndiyo maana wakakimbilia nje na kufanikiwa kuwanasa. Hizi ni tambo za kijinga. Hakuna usahihi wowote wa mtu kutembea na ‘mali’ za watu.
Je, wewe unayesoma mada hii ukoje? Ni mke wa mtu lakini una mwanaume mwingine wa pembeni? Ni mume wa mtu, lakini una kimada wako wa nje? Kuna mke wa mtu anakutega kimapenzi au mume wa mtu anakusumbua akikutaka?
Uko kundi gani? Kujua ulipo, angalau kutakupa nafasi ya kuingia katika kipengele cha pili, ambacho ni kujifunza juu ya yote hayo. Rafiki zangu, najua kuna baadhi yenu hampendi ninachokiandika hapa lakini ni tatizo kubwa kwa wengine.
Ikiwa utaweka ubongo wako tayari kujifunza, kuna kitu utakipata kupitia mada hii. Zipo athari unazoweza kuzipata ukiwa katika uhusiano na mke/mume wa mtu.
UNAPOTEZA MALENGO
Kwanza kabisa, hakuna malengo unayoweza kutengeneza na mke au mume wa mtu. Tayari mwenzako yupo kwenye ndoa yake, kwa hiyo kuwa naye hakuwezi kubadilisha matokeo (hasa kama ana ndoa ya mke mmoja).
Sana sana unapoteza muda wako na kuziba bahati ya kuingia katika ndoa yako peke yako. Huwezi kuwa na malengo yoyote kwa kuwa katika uhusiano na mtu mwenye ndoa yake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment