Sunday, March 18, 2012

Pingamizi La Upumuaji Usingizini (Obstructive Sleep Apnea)

usingizi mgumu
Pingamizi la upumuaji usingizini ni hali ya kushindwa kupumua kwa kutumia pua au mdomo kwa muda wa sekunde 10 wakati mtu akiwa amelala. Tatizo hili hutokea zaidi ya mara 30 katika hatua mbili za vipindi vya usingizi vinavyojulikana kitaalamu kama Rapid Eye Movement na Non Rapid Eye Movement.
Rapid Eye Movement Sleep ni kipindi kimojawapo cha usingizi wa kawaida ambacho huambatana na macho kucheza cheza yaani mtu anakuwa yupo usingizini huku macho yake yakicheza cheza. Kwa kawaida wakati mtu amelala hupitia hatua hii mojawapo ya usingizi na hutokea mara 4-5 katika usingizi, mwanzoni REM ikitokea kwa muda mfupi sana na mwishowe kipindi hiki kukawia kwa muda mrefu hasa inapokaribia asubuhi. Inakisiwa REM huchukua asilimia 20-25 ya usingizi wa mtu mzima yaani dakika 90-120 kwa ujumla.
Non Rapid Eye Movement Sleep ni hatua ambayo mtu anakuwa amelala lakini hapitii hatua ya REM, hivyo kumfanya kutochezesha macho, kuota ndoto ni nadra sana kwa wenye kupata hatua hii, akili huwa katika hali njema kabisa (mindset is more organized) viungo vya mwili wake kutolegea (muscles not paralyzed) ndio maana mtu anaweza kutembea huku akiwa usingizini (sleep walk).
Tatizo la pingamizi la upumuaji usingizini huathiri zaidi wanaume kuliko wanawake.
Watu gani wako kwenye hatari ya tatizo hili?
• Unene uliopitiliza (Obesity)
• Shinikizo la damu (Hypertension)
• Moyo kushindwa kufanya kazi vizuri (Congestive Cardiac Failure)
• Matatizo katika mishipa ya damu ya moyo (Coronary Heart Disease)
• Unyongovu (Depression)
• Magonjwa sugu katika mfumo wa upumuaji (Chronic Obstructive Pulmonary Disease)
• Unywaji pombe kupita kiasi
• Uvutaji sigara kupita kiasi na matumizi ya madawa ya kulevya (ilicit narcotics)
• Historia ya mwana familia kuwa na tatizo hili.
• Watumiaji wa dawa zifuatazo: Barbiturates, Benzodiazepines, Ethanol,hypertensive and diabetic treatment----kwa kifupi dawa za usingizi, shinikizo la damu na kisukari
Dalili na Viashiria
• Kula zaidi kipindi cha mchana
• Kukoroma
• Ushuhuda wa mwenzi wako – wakati wa pingamizi la upumuaji au mitweto
• Kukosa usingizi kipindi cha usiku
• Uchovu
• Kuamka usiku kwenda kukojoa mara kwa mara
Vipimo Vya Uchunguzi
• Polysomnogram
• Actigraphy
Matibabu:
1. Muendelezo chanya wa shinikizo katika mfumo wa hewa
2. Matibabu ya matatizo yanayoweza kupelekea kupata tatizo hili mfano kupunguza uzito kwa wale wenye uzito uliopitiliza, kutibu shinikizo la damu, kupunguza unywaji wa pombe na uvutaji sigara.

No comments:

Post a Comment