 Watu wengi ambao wako kwenye uhusiano wanalalamika kuwa wenzi wao  hawawaoneshi upendo kama ilivyokuwa siku za mwanzo za uhusiano wao.  Wanaeleza kuwa wanaona uhusiano wao unalegalega na mapenzi yanapungua  taratibu kama barafu iyeyukavyo juani.
Watu wengi ambao wako kwenye uhusiano wanalalamika kuwa wenzi wao  hawawaoneshi upendo kama ilivyokuwa siku za mwanzo za uhusiano wao.  Wanaeleza kuwa wanaona uhusiano wao unalegalega na mapenzi yanapungua  taratibu kama barafu iyeyukavyo juani.Ili kuepuka yote haya, hauna budi kujifunza njia za kuwasha upya moto wa upendo kila wakati kwa kuongeza ukaribu (intimacy) kati yako na mwenzako. Zifuatazo ni mbinu zitakazokusaidia:
Kucheka pamoja
Kicheko ni mlango wa ukaribu, kama mwaweza kuchaka pamoja basi mwaweza kulia pamoja, na hapa mwaweza kuaminiana zaidi katika kuwasiliana hisia zenu, kama waweza kuitofuta furaha katika kila kitu basi unaweza kupenya katika vyote. Usiwe mgugu na mwenye msimamo mkali katika kila kitu. Jifunze kujizuia pale unapoanza kuelekea kwenye kukasirika na badala yake tumia kucheka kama mlango wa kutokea. Kama utaanza kujizoeza hivi ukiwa nyumbani, taratibu utaweza ukiwa ofisini na hata kwingine kokote.
Jifunzeni kutiana moyo
Kila mmoja awe msaada na tegemeo kwa mwenzake. Jifunze kumtia moyo na kumwezesha mwenzako. Sikiliza na kufuatilia vile mwenzako afanyavyo au apendavyo.
Onyesha heshima katika vitu hivyo pia. Kila upatapo nafasi mpongeze mbele za watu au hata unapokua nae peke yenu. Mjenge mwenzako mbele yaw engine na kubali pongezi zote za mafanikio yenu zimwendee yeye. Mruhusu mpenzi wako ajue kuwa una mkubali katika kila afanyalo. Zaidi tunavyo wainua wapenzi wetu ndivyo wanavyotuthamini na kutunyangua na sisi pia.
Jifunzeni kupenda kugusana
Nguvu ya mguso wa ukaribu kamwe haiwezi kulinganishwa na chochote. Lazima mjifunze kujenga tabia ya kugusana mara mpatapo nafasi sio tu mnapokuwa mmelala. Kugusana huku ni pamoja na kushikana mkono mkiongea au mkitembea, kukumbatia bega, kugusa au kuchezea nyewele za mwenzako na njia nyingine zozote za kuonyesha ukaribu kimwili. Wengi wetu huweza kufanya haya kidogo tunapokuw peke yetu na kamwe sio mbele ya watu, Je, ni aibu, nidhamu mbaya? Dhambi?
Kugusana ndiyo mwanzo wa kuamsha hisia za kuhitajiana, (hebu jiulize kisirisiri, lini uligusana na mwenzako nje ya chumba?). Kumgusa umpendaye hukuzuia kutowaza kumgusa yeyote katika ulimwengu uliojaa wengi walio wapweke.
Mguso huu wa upendo haumaanishi mguso wa tendo la ndoa, ingawa  pia ni vyema kujifunza kuijenga lugha ya mguso wa  tendo la ndoa katika  uhusiano wenu.
Zungumzeni hisia zenu
Kati ya vikwazo vikubwa  katika ustawi wa uhusiano mengi hususan ya wanandoa ni kutokuwepo kwa  majadiliano. Lazima wapenzi wajifunze kuzungumza kuhusu hisia zao. Kama  vile maisha yasivyo na ukamilifu, uhusiano na hata ndoa pia hazina  ukamilifu.  Mpenzi wako hayuko kamili na wala wewe pia siyo mkamilifu.  Jifunze kuzungumza na umpendaye jinsi unavyojisikia na nini  kinachokusumbua. Kuendelea na migogoro isiyosuluhishwa husababisha moyo  kuwa baridi juu ya mwenzako. Jiwekeeni muda kila wiki wa kutoka ili  kuzungumza mambo yenu. Mwambie umpendaye yapi yanayojiri kila siku na  zipi ni changamoto zako mkiweza kujifunza kuwekeza katika muda wa kuwa  pamoja taratibu hata muda wenu wa maongezi ya simu utaongezeka.
Samehe na kubali kusamehewa
Kamwe  tusiache maumivu na machungu yatawale uhusiano wetu. Lazima tujifunze  kuwasamehe tuwapendao na kujisamehe sisi pia. Kutofautiana katika  uhusiano kupo sana, na lazima tuwape tuwapendao nafasi ya kuelezea vile  vinavyowaudhi dhidi yetu. Kila hisia za mmoja wetu zina umuhimu. Huwezi  kujiona vile ulivyo, mruhusu mwenzako akwambie yanayomuumiza na  msameheane.
Linda mwonekano wa mpenzi wako
Mara nyingi hatari hii hutokea  tunapokuwa katika mizunguko ya huku na huko. Ukaribu na mpenzi wako  hauendelezwi tu bali unalindwa. Mwonekano wetu lazima uwe halisi na siyo  bandia . Vile tunavyoviona katika tamthiliya na filamu siyo ukaribu  ulio halisi. Kama tunataka tuonekane sawa na vile tunavyowaona wengine  wanavyopendana basi tunakosea na kujizuia kuwa na mtazamo bora katika  uhusiano wetu. Ukianza kupata  ukaribu wa kweli baina yako na mwenzako,  utapoteza hisia ya kuhitaji ukaribu huo na mwingine yeyote, na badala  yake utaanza kuulinda ukaribu mlionao.
Lengo liwe kuvitafuta vile  vyote mpenzi wako alivyonavyo ambavyo ni kukuza ukaribu wenu. Mwenzako  awe ndiyo mtu wa muhimu kuliko wote katika maisha yako.
 
 




 
No comments:
Post a Comment