Matatizo ya kufanya mapenzi au kujamiana kwa wanawake yanatambulika kama tatizo linalojirudia kwa muda mrefu ambapo huathiri mzunguko wa tendo la kujamiana (kusisimka, kufikia kilele, kurudia) na hivyo kusababisha msongo wa mawazo au kuharibu uhusiano wa mwanamke na mpendwa wake. Tatizo hili huathiri asilimia 43 ya wanawake wa rika zote duniani na huonekana sana kwa wanawake wenye umri kati ya 45-64.
Visababishi vya tatizo hili kwa wanawake ni;- Msongo wa mawazo – Asilimia kubwa ya tatizo hili linaweza kutokea kutokana na msongo wa mawazo ambapo huchangiwa na ugumu wa maisha (uchumi), matatizo katika uhusiano (ugomvi, kutoelewana, kutoaminiana au kukosa uaminifu katika uhusiano {infedility} nk) na magonjwa mbalimbali.
- Kupungua au kukosekana upendo/mapenzi katika uhusiano au ndoa
- Kujifungua mtoto – Hii ni kutokana na homoni aina ya prolactin kuwa katika kiwango cha juu wakati mama ananyonyesha, homoni hii pia hufanya kazi ya kumfanya mtu kuridhika baada ya tendo la ndoa/kujamiana kwa kuingiliana na ufanyaji kazi wa homoni/kichocheo chengine kinachojulikana kama dopamine (ambayo ndio humfanya mtu kufikia kilele wakati wa kujamiana). Mbali na kunyonyesha, homoni ya prolactin pia huongezeka wakati mtu amelala (usingizi mzito au REM sleep), wakati wa alfajiri, baada ya kufanya mazoezi, kula,baada ya tendo la kujamiana, baada ya upasuaji mdogo na hata baada ya kupata degedege. Sababu nyengine ya kuongezeka kiwango cha kichocheo hiki cha prolactin ni kuwa na saratani katika ubongo (anterior pitituary tumors). Dalili za saratani hii ni pamoja na kutonyonyesha vizuri kwa mama, kukosa hedhi, ugumba kwa wanawake na uhanithi kwa wanaume (impotence).
- Kupungua mzunguko wa damu katika tupu ya mwanamke na hivyo kusababisha maumivu wakati wa kujamiana.
- Hypothyroidism – Matatizo ya homoni ya tezi la koo, huonekana sana kwa wanawake kuliko wanaume.
- Utumiaji wa vidonge vya kupanga uzazi au vya majira kwa muda mrefu
- Unywaji pombe kupindukia – Kinyume na fikira potofu za watu wengi ambao huamini kwamba unywaji pombe kali huongeza hamu ya kujamiana au kupunguza uzito lakini ukweli ni kwamba pombe kali au kilevi cha aina yoyote hupunguza hamu ya kujamiana na pombe huongeza uzito na kusababisha utapia mlo.
- Ugonjwa wa kisukari
- Uvutaji sigara
- Ujauzito – Kutokana na mabadiliko katika mfumo wa homoni au vichocheo wakati wa ujauzito, na pia kutokana na mabadiliko ya maumbile ya wanawake wakati huu na hivyo kuchangia kutojiamini kwa mwanamke.
- Uzito uliopitiliza (obesity)
- Ugonjwa wa mifupa (arthritis)
- Utumiaji madawa ya kulevya
- Madhara katika neva inayohusika na kuongeza msisimko wakati wa kujamiana (pudendal nerve damage) wakati wa upasuaji wa kuondoa mfuko wa uzazi kwa mwanamke mwenye matatizo ya uzazi au katika mfuko wa kizazi.
- Madhara ya dawa – Kama dawa za kutibu shinikizo la damu, antidepressant medication, dawa za saratani nk.
- Uchovu – Kuzidiwa kwa mwanamke na majukumu ya kulea mtoto/watoto, kazi na kumhudumia mume wake hivyo kusababisha uchovu.
- Ugonjwa wa moyo
- Saratani ya aina yoyote ile
- Kuwa na wasiwasi (anxiety), depression nk.
- Historia ya kubakwa, au kupata maumivu wakati wa kujamiana hapo awali kutokana na mwanamke kutokuwa tayari kujamiana au kutotayarishwa vyema kabla ya kujamiana au magonjwa ya zinaa.
- Tatizo la vaginismus – Hii ni tatizo ambalo husababisha tupu ya mwanamke kuwa ndogo wakati wa kujamiana na hivyo husababisha mwanamke kupata maumivu wakati wa kujamiana.
- Kupenda inataneti kupita kiasi (addiction) – Katika tafiti mpya iliyofanyika mwaka huu nchini marekani, imeonyesha ya kwamba kati ya ndoa 6,000 zilizovunjika asilimia 57 zimesababishwa na mwenza mmoja au wote kupenda kuchat au kutumia intaneti kupita kiasi na hivyo kusababishwa msisimko kupotea kati ya wenza wawili na hatimaye mwisho ni kupungua uwezo au hamu ya kujamiana.
- Wanawake ambao wana historia ya kupungua hamu ya kujamiana
- Wale ambao wamefanyiwa upasuaji wa kuondoa mayai yao ya uzazi kutokana na sababu mbalimbali
- Wanawake ambao waliofika umri wa kuacha kupata hedhi (menopause- miaka 42-58)) na kupata dalili mbalimbali kama kutokwa na jasho usiku, kukosa usingizi mzuri na depression.
- Msongo wa mawazo kama nilivyoeleza hapo juu
- Kupungua au kukosekana upendo/mapenzi katika uhusiano/ndoa
- Unywaji pombe kupindukia kama nilivyoeleza awali
- Utumiaji wa dawa za kulevya
- Uvutaji sigara – Hupunguza kiwango na uzito wa shahawa kwa wanaume. Uzito wa shahawa (concentration of spermatozoa in semen) hupungua kwa asilimia 22-57 kwa wale wanaovuta sigara. Uwezo wa shahawa kuogelea kwenye mirija ya uzazi ya mwanamke pia nao hupungua kwa asilimia 20 kwa wale wanaovuta sigara ikilinganishwa na wale wanaume wasiovuta sigara.
Pia uvutaji sigara hupunguza vichocheo aina ya testerone, growth hormone, na nk.Wanaume wenye kiwango kidogo cha testerone huwa na tatizo la kupungukiwa uwezo wa kujamiana na kiwango kidogo cha shahawa.Uvutaji sigara hupunguza mzunguko wa damu unaopita/kwenda kwenye moyo na kwenye uume na hivyo basi kumfanya mwanamume kushindwa kusimika na kupata tatizo la kupungua uwezo wa kujamiana (vascular impotence).
Katika tafiti zilizofanyika, asilimia 97 ya wale waliogunduliwa na tatizo la vascular impotence walikuwa wavutaji sigara na katika tafiti nyengine asilimia 87 ya wale wenye tatizo hili la vascular impotence walikuwa pia wavutaji sigara. Katika tafiti iliyohusisha wapenzi 290 hapo mwaka 1999, ilionyesha ya kwamba wanaume ambao walikuwa wavutaji sigara walifanya tendo la ndoa na wake zao mara 6 tu kwa mwezi mzima na wale ambao hawakuwa wavutaji sigara walifanya tendo la ndoa mara mbili zaidi ya wale wavutaji sigara.
Uvutaji sigara, huusishwa pia na kuongezeka kwa chembechembe nyeupe za damu kwenye shahawa ambazo kwa kawaida hutolewa kukiwa na ugonjwa ndani ya mwili, chembechembe hizi ambazo zinakuwepo kwa wingi kwenye shahawa pasi na kuwepo kwa ugonjwa, hupunguza uwezo wa shahawa kuingia na kuungana na yai (ovum) kutoka kwa mwanamke na hivyo kusababisha kutotunga kwa mimba.
- Ugonjwa wa kisukari
- Uzito uliopitiliza (obesity) – Kutokana na kuongezeka kwa mafuta ambayo husababisha mishipa ya damu inayopeleka damu kwenye moyo na uume kuwa midogo na kupungua uwezo wa kujamiana. Kupungua uwezo wa kujamiana au kufanya mapenzi kwa wanaume ni ishara mojawapo ya ugonjwa wa moyo na kiharusi.
- Hypothyroidism – Matatizo ya vichocheo katika tezi la koo
- Kuwa na wasiwasi (anxiety), depression
- Kupenda mambo ya intaneti kupita kiasi (addiction to internet) kama nilivyoeleza awali.
- Umri – Kuanzia miaka ya 40,kiwango cha kichocheo aina ya prolactin huongezeka na kusababisha kuongezeka kwa kichocheo chengine aina ya dihydro-testerone ambacho husababisha tezi dume kuongezeka na hatimaye kupunguza uwezo wa kusimika kwa mwanamume (rudia makala ya kuvimba tezi dume – Benign Prostate Hyperplasia, BPH)
- Madhara katika neva inayohusika na kusimika kwa uume (pudendal nerve damage)
- Kuendesha baiskeli muda mrefu (kwa kipindi kimoja) – Hii hugandamiza neva na mishipa ya damu inayopeleka damu kwenye uume na kusababisha tatizo la kupungua kwa uwezo wa kusimika kwa mwanamume kwa muda tu (temporary).
Kabla ya kufanya vipimo vya uchunguzi, Daktari atachukua historia ya mgonjwa inayohusisha matumizi ya dawa aina mbalimbali, historia ya magonjwa, pamoja na kuangalia dalili za magonjwa mbalimbali. Vipimo vya uchunguzi vitatokana na historia ya mgonjwa ambayo Daktari ameweza kuipata kutoka kwake. Vipimo hivyo vinaweza kuwa
- Kuangalia magonjwa kwenye tupu ya mwanamke au kama kuna bakteria aina yoyote.
- – Kuangalia magonjwa ya zinaa
- Vipimo vya mkojo (urinalysis)
- Kipimo cha kuangalia mabadiliko yoyote kwenye tupu ya mwanamke (physical changes, thinning of genital tissues, decreased skin elasticity and scarring)
- Kumpima mgonjwa akili ili kuweza kutambua kiini cha tatizo
- Vipimo vya vichocheo kama T3, T4, testerone level, growth hormone, prolactin hormone nk.
- Semen analysis – Kipimo cha kuangalia shahawa, wingi wake (volume), kiwango chake, mvutano wake (liquefaction time), sperm count, maumbile yake (sperm morphology), PH yake, uwezo wake wa kuogelea (sperm motility), kiwango cha sukari na chembechembe nyeupe za damu.
- BMI – Kipimo cha kuangalia kama mtu anauzito unaolingana na urefu wake pamoja na umri wake au ana uzito uliopitiliza
- Vipimo vya ugonjwa wa shinikizo la damu – Kwa wale wenye shinikizo la damu au dalili zake au wanaotumia dawa za shinikizo la damu
- Vipimo vya ugonjwa wa kisukari – Fasting Blood Glucose test, Oral Glucose Tolerance Test (OGTT), glycosylated hemoglobin (Hb A1C) rudia makala ya Kisukari kwenye tovuti ya Tanzmed.
Tiba ya tatizo hili inahusisha
1.Kubadilisha mfumo wa maisha
- Kufanya mazoezi mara kwa mara – Mazoezi huongeza stamina, hupunguza uzito,humfanya mtu kuwa na umbile zuri, furaha na kuongeza ufanisi wakati wa kujamiana
- Kupunguza msongo wa mawazo kwa kukubali kwamba tatizo lipo baina ya wanandoa na hivyo kutafuta suluhu pamoja na kuacha ugomvi. Matatizo ya kimaisha (fedha, nk) lazima yatafutiwe ufumbuzi.Kufanya mazoezi ya pelvic muscles kwa kufanya kama unazuia mkojo wakati unahisi haja ndogo na kuhesabu kutoka moja hadi tano, baada ya tano pumzika na halafu rudia. Haya mazoezi (kegel exercise) huongeza uwezo wa kujamiana kwa wanawake
- Zungumza na mwenza wako – Malumbano na matatizo ni vitu vya kawaida katika uhusiano wowote, ni vizuri kwa wenza kukaa pamoja na kuzungumza matatizo yao, kuwa wakweli, waaminifu, kuaminiana, kujaliana na kuzungumza juu ya tendo la ndoa kwa pamoja. Ni vizuri kila mmoja kuainisha vitu anavyopenda na asivyopenda kufanyiwa wakati wa kujamiana. Pale inapotokea mmoja hajapendezwa au kufurahishiwa na uwajibikaji au ufanisi wa mwenzie basi hana budi kutumia lugha nzuri kutafuta kiini cha tatizo na kulitafutia ufumbuzi.
- Weka mazingira mazuri na muda wa kufanya tendo la ndoa na mwenza wako ili mupate kudumisha uhusiano wenu
- Ongeza msisimko katika uhusiano wenu kwa kujaribu aina au staili mbalimbali wakati wa kujamiana, kubadilisha muda wa kufanya mapenzi (sio usiku tu hata asubuhi, mchana) au sehemu tofauti na ile muliyoizoea wakati wa kufanya mapenzi (sio kila siku kitandani)
- Kupata ushauri nasaha kutoka kwa wataalamu wa mambo ya uhusiano, marriage counsellors na hata madaktari wa magonjwa ya akili kwani hawa ni weledi zaidi katika kazi yao.
- Kutibu ugonjwa ambao ni kiini cha tatizo hili – Kisukari, magonjwa ya moyo, magonjwa ya zinaa nk.
- Daktari kumbadilishia mgonjwa dawa zinazoleta madhara kama ya msongo wa mawazo, depression nk.
- Kutibu tatizo la depression na anxiety
- Kutumia dawa au jelly zinazolainisha tupu ya mwanamke wakati wa tendo la ndoa kwa wale wanaopata maumivu au kupunguza tupu kuwa kavu au kuwasha (irritation).
- Tiba ya homoni au vichocheo – Estrogen Replacement Therapy (ERT) and androgen therapy.
- Dawa aina ya Yohimbine Hydrochloride
Ikumbukwe ya kwamba vyakula hivi sio tiba mbadala bali husaidia tu kupunguza ukubwa wa tatizo hili la kupungua au kukosa hamu ya kufanya mapenzi na kuboresha kwa wale ambao hawana tatizo hili na hivyo kudumisha uhusiano.
- Kitunguu swaumu – Kitunguu swaumu kina kemikali aina ya allicin ambayo huongeza mzunguko wa damu kwenda kwenye uume, huongeza hamu ya kufanya mapenzi na utolewaji wa shahawa.
- Habat al soda (black caraway seeds) – Mafuta,mbegu,au unga wa habat soda kama wengi wanavyoita na ambazo zimetumika kwa miaka mingi sana kupunguza tatizo hili na waandishi wengi wameeleza umuhimu wake. Tumia kidogo kwenye chai au maji ya uvuguvugu mara mbili kila siku. Mbegu hizi hupatikana kwa wingi katika nchi za asia kama Saudi Arabia, Syria, Iran, Dubai (UAE), na hata Misri, Tanzania (Dar-es-salaam katika maduka ya dawa za asili ya kariakoo, mbagala, na Zanzibar)
- Celery au giligilani – Hii huchochea hamu ya tendo la ndoa kutokana na uwepo kwa wingi wa kichocheo aina ya androsterone.
- Ndizi – kuwepo kwa wingi kwa enzyme aina ya bromelain na madini ya potassium huongezeka msisimko wa kufanya mapenzi kwa wanaume.Potassium pia hupatikana kwenye tikiti maji ambalo pia lina kemikali aina ya arginine ambayo huongeza wingi wa damu katika mishipa ya damu na hivyo kusaidia katika kusimika kwa uume.
- Parachichi – Huwa na kiwango kikubwa cha folic acid ambayo huvunjavunja protini. Vitamini B6 kwenye parachichi huchochea kutengeza kichocheo aina ya testerone kwa wingi.
- Mayai – Mayai yana kiwango kikubwa sana cha vitamini aina ya B5 na B6, ambazo husaidia kuleta usawa wa viwango vya vichocheo mwilini na kupunguza msongo wa mawazo.
- Nyanya/Tungule (tomatoes) – Zina kiwango kikubwa cha virutubisho aina ya bio-active phyto-nutrients, lycopene, na beta carotene ambazo husaidia kuleta damu kwa wingi kwenye uume na hivyo kusaidia kusimika kwa uume
- Chocolate – Ina kiwango kikubwa cha kemikali aina ya theobromine na phenylethylamine ambazo huongezeka hamu ya kufanya mapenzi.
- Vitamin A – Husaidia katika kuweka usawa wa vichocheo vya mapenzi (sexual hormones). Vyakula venye wingi wa vitamin hii ni pamoja na karoti, maini,tikiti maji, spinach, maziwa nk.
- Vitamin B complex – Huongeza kiwango cha kichocheo cha testerone ambacho husaidia katika kuongeza ufanisi wa tendo la ndoa kwa wanaume na wanawake. Vitamini B complex hupatikana kwa wingi kwenye ndizi, viazi tamu, lentils, mboga za majani, parachichi (avocado), mayai, nyama aina ya tuna, bata mzinga, maini nk.
- Vitamin C – Tafiti zilizofanywa karibuni zimeonyesha ya kwamba vitamini C inapotumiwa pamoja na vitamini nyengine, husaidia L-enantiomer ya ascorbic acid kudhibiti msongo wa mawazo, wasiwasi (anxiety), utolewaji wa homoni ya prolactin na huongeza mzunguko wa damu pamoja na kutolewa kwa kichocheo cha aina ya oxytocin na hivyo kuongeza ufanisi wa tendo la ndoa. Vyakula venye vitamin C ni ndimu, chungwa, limao, brussels sprouts, mapera, tikiti maji, nyanya, broccoli, kiwi, papai, strawberries, pilipili hoho na pilipili mbuzi nk.
- Vitamin E – Husaidia kudhibiti matamanio ya mwanamume pamoja na kusimika kwa uume kutokana na uwepo wa vichocheo aina androgens na estrogen ambavyo huchanganyikana na homoni za mayai (ovarian hormones) na testerone. Vyakula venye vitamin E ni pilipili hoho, nyanya, olives, tunda aina ya kiwi, papai, mafuta ya alizeti, karanga nk.
- Madini ya Zinc – Muhimu katika utengenezaji wa testerone
- Madini ya selenium – Huongeza uwezo na nguvu ya kufanya mapenzi kwa wanaume.
- Madini ya magnesium na calcium – Calcium ni muhimu katika kusaidia ufanisi wa kufanya mapenzi. Huweka mawasiliano ya karibu kati ya ubongo na tezi zinazotoa vichocheo vya mapenzi pamoja na kusaidia katika ufanyaji kazi wao. Madini ya magnesium husaidia kuondoa madhara ya madini ya calcium katika kusaidia kuhimili kusimika kwa uume. Vyakula venye madini ya calcium ni maziwa, mtindi, cheese, siagi, chungwa, almonds, walnuts, maharage meupe, ice cream, chocolate nk.
- Cinnamon stick (mdalasini) na Asali (Honey) – Mchanganyiko wa vitu hivi viwili husaidia sana katika kuongeza ufanisi kwa wale wenye tatizo hili. Jinsi ya kuandaa, chukua mdalasini robo na changanya na asali nusu lita kisha weka kwa siku tatu, baada ya siku tatu anza kunywa kwa kutumia kikombe cha kahawa mara tatu kwa siku kwa muda wa wiki mbili (kama utatumia mdalasini nusu basi changanya na asali lita moja).
No comments:
Post a Comment