Sipendi Ndevu Zake
Usafi na Ngono
Jinsi ya Kusaidia Mmeo ktk Ngono
Ngono ni sanaa
"Mimi nilitaka kukuuliza hivi ndevu zina raha gani? Ni mama kijana wa miaka 27 nipo kwenye ndoa kwa miaka 6 sasa hivi na watoto watatu na mwengine yupo njiani. Mume wangu ananifugia mindevu kitu ambacho nakichukia.
Nimeshamuambia vya kutosha aliniambia hana mda wa kushave, niliamua kumtafutia mashine awe anashave mwenyewe angalau apendeze kama wanaume wenziwe, yaani bado pia hajamua kufanya hivyo.
Alafu haziweki kiusafi, hicho ndio kinaniuma hasa, mbaya zaidi hunyoa para anabakisha mi ndevu some time hutamani nipige kelele naona raha nnapowaona rafiki zake wamependeza roho inaniuma sana.
Inapokuja kwenye masuala ya sex hio ndio inanitia kinyaa, kwa sababu kwanza hupenda kwenda chumvini basi akitoka hapo yale mandevu yanavotisha then hutaka kunikiss na mimi, mwili wote hunisisimka kama angekuwa hana hiyo midevu mimi simind najua mapenzi ni kila kitu lakini ile midevu inavyokua wet then hunipaka paka nayo akiwa ananikiss mwilini roho inaniuma sana si enjoy hata kidogo.
Au akilala kama nitamuamsha kwa bahati mbaya basi utakuta imejaa midenda tena hii tabia anayo mda mrefu sasa, he doesnt care about me, hajali kwamba nini napenda kuhusu yeye anachojali ni yeye mwenyewe kitu kinachomueka yeye happy kwake nafanya, wewe ukipenda usipende yeye hana mpango huo wa kujali.
Hicho ndio kinaniudhi, yeye aliniambia vitu vingi ambavyo hapendelei mimi niwe navyo kwa vile nampenda vingi niliachana navyo kwani sikupenda kumuudhi lakini kwa upande wake yeye ninachomuambia hatekelezi nimechoka kwa kweli.
Mume wangu nampenda sijui cha kufanya ili nae awe smart kama wenzie, nimejaribu kupuuzia mambo mengi na kumuacha kama alivyo afanye anavyotaka labda atachange naona ndio anazidi naombeni ushauri wanu hivi ndevu zina raha gani na nifanyeje ili nizizoee. Mwanaume na nampenda ila hiyo ndio karaha yake."
Jawabu:Asante , unajua umenifanya nicheke(samahani). Sina uhakika nini hasa faida ya ndevu kwa wanaume, ila natambua kuwa kuna baadhi ya wanawake wanapenda wanaume wenye madevu ili kupata ule mkwaruzo wanapowabusu au kuwachezea-chezea wapaokuwa wakekaa mahali wametulizana.....kama ambavyo baadhi hupenda kuchezea nywele za kifuani, kichwani, sirini au kwapani.
Kule kwetu tunafundishwa mambo mengi ambayo yakifanywa na kuwa kawaida inakuwa rahisi kugundua kuwa mumeo anapoteza "interest" kwako kutokana nakujisahau kwako hali inayoweza kusababisha yeye kutafuta akikosacho nje.
Na njia kuu mbili za kutambua hilo ni mabadiliko ya uvaaji na anavyojiweka( kwa sababu ni kazi yako, ikibadilika utajua kuna walakini), vilevile kupenda kula "kwa watu" na sio chakula chako(ni wajibu wako kujifunza mapishi mengi tofauti na kutoruhusu mumeo ale kwa watu).....hii ikitokea kwenye ndoa basi unatakiwa kuchukua hatua madhubuti na za haraka kurekebisha makosa.
Pia tunaambiwa kuwa, mume wako anapokuwa mataani na wewe unakuwa pembeni yake (hata kama haupo), kama sio smart lawama ni kwa mkewe kwamba hamjali mumewe.....mumeo nahitaji muongozo wako na ushirikiano wako ili kuwa vile unavyotaka ili aendelee kukuvutia.
Unadai akitoka chumvini na ile midevu anatisha inamaana akitoka huko anatoka na Utoko?? otherwise hawezi kutisha kwani ule ute hauna rangi na actually hauonekani hata ukiwa kwenye ndevu ni kama maji tu, linapokuja suala la kukubusu baada ya kutoka huko nitakuelewa kwa vile kutakuwa na unyevunyevu kwenye ndevu zake lakini zaidi ya hapo hakuna cha kutia kinyaa ukizingatia uke ni wako na huna budi kuupenda(acha kujishusha Binti mzuri wewe).
Umeeleza kuwa, ulimuambia vya kutosha kuhusiana na kunyoa ndevu zake kwa vile hazikufurahishi na yeye akakujibu kuwa hana muda.....that's a real man right there! Mwanaume kamili huwa hazunguuki ili kukuambia ukweli au anataka nini? anasema moja kwa moja tofauti na wanawake wanasema hiki wakati wanamaanisha kile.
Mumeo amekuambia moja kwa moja kwamba tafuta muda na umnyoe na sio kwenda mununulia mashine ili ajinyoe kama ulivyodhania. Pamoja na kuwa mashine itarahisisha kitendo na kuwa cha haraka bado suala la kutokuwa na muda liko pale pale.
Kutokana na maelezo yako sidhani kuwa mumeo anapenda kuwa na madevu, hivyo basi ukitafuta muda na ukawa unamnyoa au kupunguza kiasi kile unachopenda Mf:-Kila Jumapili, kumsaidia kuziweka vema kila asubuhi mara baada ya kutoka kuoga/koga, kama ni kipilipili kuna "cream" za kuzinyoosha kimtindo unaweza kutumia (usiwaona akina Will Smith ndevu zao zinavutia ukadhani walizaliwa hivyo....ni mapoudaa I mean creams za kiume za kunyoosha nywele) ili kuhakikisha kuwa wakati wote anaonekana smart the way you like him to be.
Kumbuka kuwa wewe ndio mkewe na yeye kukuvutia ni muhimu hivyo make an effort na msaidie sio kunyoa tu, hata kumnunulia/chagulia mavazi mazuri na ya kisasa ili apendeze, natambua kuna baadhi ya wanawake wanaogopa kuwapendezesha waume zao wakihofia watavutia wanawake wengine nje....hey kama mume wako anavutia watu wengine kutokana na juhudi zako wewe mkewe ni jambo la kujivunia sana.
Hali kadhalika kwa wanaume...kama mkweo unamtunza vema mkeo, umamruhusu kutilia viwalo fulani vya kuvutia na anavutia wanaume wenzako unapaswa kujivunia kuwa una a "hot wife" na kujipa 5 kwa kazi nzuri.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment