Ngono baada ya kujifungua
Kungonoana au kungonoka na kufurahia tendo baada ya kujifungua inategemea zaidi na wewe mwenyewe (uponaji wako) na lini unadhani uko tayari vilevile ushirikiano wa kutosha kutoka kwa mume/mpenzi wako wakati unaendelea na uponaji baada ya kutoa kiumbe kipya duniani.
Ni hali ya kawaida kabisa kwa mwanamke kutokujiskia (kutonyegeka) au kutaka ngono kwa wiki chache tangu ujifungue na hii inatokana na kusubiri dam ya uzazi kuisha bila kusahau yale maumivu kule ukeni (sore) kupungua au kupona kabisa.
Ili kufanikisha uponaji wa haraka inategemea na wewe mwenyewe utakavojisaidia na kufuata ushauri wa Wakunga na Daktari wako bila kusahau njia unayotumia "kusababisha" uponaji wa haraka.
Njia ambayo wanawake wengi wa kiafrika wanaitumia ni maji ya moto na utumiaji huu wa maji unatofautiana na hii inategemea na Asili yako (kule utokako) kwani kuna baadhi huongezea aina ya majani (kama dawa) ili kusaidia uponaji wa mama mzazi, wengine huchanganya maji hayo ya moto na unga unaotokana na aina fulani ya mizizi nakadhalika......Afrika tuna madawa mengi asilia ambayo yanafanya kazi nzuri kabisa.
Hizi ni aina 3 za utumiaji wa maji moto nizijuazo.
1-Kukandwa/mwagiwa maji ya moto ukeni-Mwanamke hukalishwa kwenye "kigoda" au kitini na pengine kuchutama kisha shughuli inaendelezwa na mama, mama mkwe, Shangazi, Bibi au Mume wako. Mtindo huu wa maji moto ni mzuri lakini haumalizi damu ya uzazi haraka, hivyo unaweza ukapona kwa maana "sore" kutokuwepo lakini damu ikaendelea kutoka kama ifuatavyo kwa muda zaidi. Njia hii ya utumiaji wa maji ya moto huchukua kati ya siku Arobaini mpaka miezi mitatu kupona kabisa.
2-Kukalia mvuke-Namna hii ya utumiaji wa maji mto wengi huwa hawaitumii lakini ni "the best" lakini unahitaji maji ya mto kweli kweli, husababisha uponaji wa haraka kwa vile unapokalia mvuke unasaidia kuvuta ile damu (hasa kama ni mabonge) kushuka kwa wingi hivyo ukifanya mara mbili au tatu kwa siku baada ya wiki mbili unakuwa uko tayari kwa "mizunguuko".
3-Kalia maji-Hapa sio maji ya moto bali joto vinginevyo matako yatazidi kuwa meusi hihihihihi(dont take it personal)karai au beseni au "bath" ndio hutumika, hii ni namna ambayo baadhi ya wanawake huitumia lakini ni ya kivivu na pia uponaji wake huchukua muda mrefu zaidi kuliko hizo mbili nilizowaeleza hapo juu.
Baadhi ya wanawake hudharau "Utamaduni" wa kutumia maji moto wakisubiri damu ishuke yenyewe na matokeo yake ni kupata maambukizo ambayo husababisha harufu mbaya sana na wakati mwingine kutokwa na usaha ukeni(wanaita kuoza)hili likitokea ni wazi kuwa itakuchukua hata mwaka kabla hujapona kabisa na kurudi kwenye "mambo" fulani hali inayoweza kusababisha uhusiano wenu kuwa kwenye wakati mgumu hasa kama mume/mpenzi wako sio mwelevu na mvumilivu.
Kama hauko "sore" sana unaweza kutumia kidole kurahisisha mabaki ya damu ya uzazi kutoka, ni kama vile nlivyokuelekeza namna ya kuondoa utoko a.k.a jinsi ya kusafisha uke.
Katika kipindi hiki mwanamke hupaswi kuharakisha mambo, nikiwa na maana kuhisi “msukumo” wa kupona haraka ili ungonoke na mumeo kwa kuhofia kuwa atachepuka, pamoja na kusema hivyo ni vema kujitahidi na kuwa karibu zaidi na mumeo/mpenzi kimapenzi na kushirikiana nae.
Sio “kudeka” kwa vile tu umezaa (kuzaa ni sehemu ya uanamke hivyo usimfanye mumeo/mpenzi wako kujihisi “guilt” as if kukumimba ilikuwa kosa wakati mlielewana...er.. let’s say matunda ya ndoa/mizunguuko).
Siku ya mwanzo kungonoka baada ya kupona kuna uwezekano mkubwa wa wewe kutopata raha au utamu na badala yake ikawa maumivu fulani hivi ambayo sio makubwa sana yaani kama yale upatayo unapo kaa muda mrefu bila kuingiziwa mtalimbo”.
Vilevile unaweza ukahitaji kilainisho cha kutosha na hapa sizungumzii mate bali Kay-Y Jell ili kukabiliana na ukavu wa uke ambao unaweza kujitokeza ktk ya “game”.
Kwa kawaida uke hujirudi kama awali ndani ya siku Arobaini au Miezi mitatu yote inategemea na uponaji wako na njia uliyotumia ili kusababisha uponaji wako.
Licha ya kuwa “sore” na damu ya uzazi kukupotezea hamau ya kungonoka au kufanya mpenzi na mume/mpenzi wako pia kuna sababu nyingine zinazoweza kupelekea wewe mwanamke mzazi kushindwa au kupoteza hamu ya kungonoka na hivyo kumkwepa Jamaa kila atakapo mambo fulani.
Baadhi ya sababu hizo ni:-
- Uchovu wa mwili na akili kutokana na kutokupata usingizi wa kutosha mishughuliko yako kama mwanamke na vilevile mama.
-Maumivu ya mshono kama ulijifungua kwa njia ya upasuaji, uliongezewa njia au ulichanika kutokana na ukubwa wa mtoto inategemea na pia atakavyokuwa akitoka.
-Kutokupata muda wa kuwa karibu na mpenzi/mume kutokana na mapenzi yako mazito kwa mtoto wako, yaani unahisi kuwa mtoto anakuhitaji zaidi kuliko baba’ke.
-Kupoteza hali ya kujiamini kwa vile unadhani kuwa mwili wako hauko kama ilivyokuwa baada ya kujifungua.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment