Tuesday, March 24, 2009

Jinsi ya kusafisha Uke wako

Jinsi ya kusafisha Uke wako!

Awali nilikuwa nikidhani kuwa kila mwanamke anapaswa na anafahamu jinsi ya kujisafisha ndani ya uke mara tu baada ya kuondolea bikira (kuanza mahusiano ya kimapenzi na hatimae ngono), lakini nimekuja kugundua ukweli kwamba wanawake wengi hawajui uke unasafishwa vipi?

Baadhi huofia kuwashwa na sabuni na wengine hudhani utokwaji wa utoko ni kawaida hivyo hawana budi kuacha kama ilivyo na badala yake hutumia “pads” ndogo au “wipes” zenye manukato ili kuzuia harufu/shombo ya uke na vilevile kuzuia uchafukwaji wa “vyupi” vyao.

Huitaji kuficha(Bali punguza) harufu ya asilia ya uke kwa kutumia bidhaa zenye mahukato hasa ukiwa na mpenzi wako kwani hiyo harufu ndio uanamke wenyewe na ikikutana na ile ya kiume ndio raha ya kufanya mapenzi na ikiwa mpenzi wako ni “aliyejaaliwa” atakuwa akiipenda harufu hiyo na hubaki akilini mwake hali inayoweza kumfanya akupende zaidi au kutoweza kufanya ngono na mtu mwingine bali wewe.

Hujawahi kusikia wanaume wanashindwa kutoka (date) wanawake wengine baada ya wapenzi wao kufariki dunia? Au mwanaume kushindwa kuendelea na maisha yake ya kimapenzi bila wewe na matokeo yake hata mkiachana lazima atarudi tu kwako….sababu moja wapo ni hiyo.

Kujiswafi ili kupunguza ukali wa shombo/harufu ya uanamke:
Utoko hujikusanya ikiwa mwili umetulia (usiku) hivyo hakikisha unajisafisha kila asubuhi kabla hujaanza kuoga.
Wengi wanatumia maji ambayo usalama wake ni wa utata, sasa ili kuepuka maambukizo hakikisha maji ya kujisafishia sehemu zako za siri yamechemshwa vizuri. Unaweza kutenganisha maji ya kuoga na ya kusafishia uke ukitaka.

*Kabla hujaguza uke wako hakikisha umesafisha mikono yako vizuri kwa sabuni (ukiweza tumia sabuni yenye dawa) na wakati huo huo pitisha sabuni juu ya uke wako ili kuondoa vijidudu kama vilikuwepo, safisha mahali hapo(juu ya uke kwa maji na hakikisha hakuna sabuni).

*Kisha kwa kutumia kidole chako cha kati, ingiza taratibu pale ambapo uume unaingia, kwa kuanzia huitaji kwenda mbali sana. Zunguusa kidole hicho taratibu huku ukijimwagia maji kwa kutumia mkono wa pili, kisha kitoe (kitatoka na weupe mzito) safisha kidole na maji yako.

*Rudia tena na sasa kiingize ndani zaidi na ukizunguushe tena (huku ukijimwagia maji) na kukitoa utaona “utoko” mwingi zaidi kidoleni, rudia hatua hizo mpaka uhakikishe kidole kinatoka bila weupe(utoko) na utahisi hali ya usafi, hakuna utelezi.

Unapojimwagia maji ukeni huku kidole kiko ndani maji huingia pia ukeni na ndio maana mwishoni kabisa utahisi umesafishika vema kabisa na utoko huo hautotoka tena siku nzima na uke wako hautokuwa na shombo kali kama ambavyo siku zote ambazo ulikuwa hujisafishi.

Kwa wale wanaotumia “bath” au “shower” unafanya kama nilivyoeleza ila tofauti ni kuwa maji yataingia vizuri zaidi ikiwa unapata “bath” hivyo hakikisha “bath” sio ya kuchangia, maji ni salama(safi), usiweke sabuni (bath cream) au bidhaa yoyote yenye kemikali kwenye “bath” yako ili kuepuka matatizo ya kiafya na maambukizo mengine.


Uke na Kusafisha Utoko

Kwa kawaida wanawake huwa wanatoa majimaji yenye uzito tofauti hali inayotegemeza zaidi mzunguuko wako wa hedhi. Majimaji hayo hujulikana kama "utoko", Utoko huu huwa ni mweupe kama maziwa na huwa na harufu ya uanamke.

Utoko huanza kutoka pale unapokaribia ukuaji/mabadiliko/kubalehe, kutokana na umri mdogo wanaokuwa nao wakati huo (hawaruhusiwi kujisafisha zaidi ya pale juu kuondoa mkojo) utoko huo husababisha rangi mbaya ya chupi zao hasa kama ni nyeupe au zina rangi ng'avu kama nyeupe n.k. pale katikati.

Jinsi siku zinavyokwenda mtoko wa utoko huongezeka uwingi. Utoko ni muhimu kwa wanawake na una kazi yake ambayo ni kusafisha njia ya uzazi na uke kwa ujumla lakini kusema hivyo sina mana basi uyaache hayo mautoko yakae chupini ei?

Usafishaji hufanyika kwa ndani na unapotoka ina maana hauna kazi tena na hivyo huna buni kuundoa kwa kujisafisha kama ambavyo wanawake wote wanafahamu jinsi ya kujiswafi.

Unapofikia umri mkubwa na kujiingiza kwenye swala la mahusiano na hatimae kuanza kufanya ngono, huo ndio wakati muafaka wa wewe kuanza kujisafisha uke wako na kuondoa utoko ili kuwa huru (shombo free), kupunguza shombo ya "uanamke" kule chini wakati wa kufanya mapenzi, kupunguza siku za hedhi (kwa kawaida unakwenda siku saba lakini kuna uwezekano mkubwa kabisa kuwa unakwenda siku nne tu) na vilevile kupunguza maambukizo ambayo yanaweza kusababishwa na ufujaji wa utoko ndani ya uke wako.

Usafi wa Matako na Uke!


Kawaida ya mwanawake sio wa Kibongo tu bali hata yule wa Ulaya,Uchina,Uarabu na Umarekani hujali zaidi ngozi ya uso na akijitahidi sana itakuwa sehemu zinazoonekana kwa urahisi kama vile shingo, mikono, viganja na ngozi ya miguu.

Lakini maeneo kama tumbo na makalio huwa havijaliwi sana (sizungumzii mkorogo hapa tafadhali) nazungumzia ile hali kawaida ya kujali ngozi na kuwa msafi ktk maeneo hayo muhimu.

Unajua mwili wako mwanamke umeumbwa kuvutia kutokana na ile “mituno” asilia inayokufanya uwe tofauti na mwanaume hapo nina maana matiti, hips na matako.

Mituno hii huvutia ukiwa umevaa nguo na kufanya mtazamaji apendezwe na kuvutiwa lakini je akiondoa hizo nguo mituno hiyo itakuwa kama vile anavyofikiria?


Utunzaji/usafi wa matako na “hips” kwa njia ya asili.


Sote tunafahamu kuwa ngozi ya maeneo hayo sio sawa na ile ya sehemu nyingine ya mwili, maeneo haya hukabiliwa na vipele Fulani hivi vigumu, baadhi hupauka kuliko na wengi hukabiliwa na michirizi.


Hakikisha kuwa unasugua sehemu hiyo ya mwili wako kwa kutumia machicha ya nazi au unga wa mmea wa liwa kusugua maeneo hayo, fanya hivyo mara moja kwa wiki kama unamudu na una senti za kununua nazi na liwa basi unaweza fanya hivyo kila siku (ila mara moja kwa wiki inatosha kabisa kukupa ulaini wa sehemu hizo na kuondoa mpauko na vipele uzembe).

Njia nyingine kwa wewe mwenye ngozi ya mafuta ni kujisugua sehemu hizo kwa kutumia pumba za maindi au unga wa dona (mahindi yaliyosagwa bila kukobolewa/ondolewa ngozi)….

Vilevile hakikisha jamaa anamwaga kwenye makalio yako wakati wa ngono sio kila siku ndani tu au kwenye kondom kwani manii huboresha ngozi ukipaka kama mafuta/lotion ikiwa Jamaa lako choyo na shahawa zake basi wewe kula mboga za majani na kunywa maji kwa wingi na wakati huohuo unayasugua mapele hayo...

Hakikisha unasafisha na maji na unamalizia kupaka mafuta/lotion kila unapomaliza kuoga au kusugua makalio yako.

Usafi wa makalio sio kwenye mapele na ukavu tu bali kuna vile vinywele hujiotea kwenye mstari wa “ikweta” kuelekea au kuzunguuka sehemu ya kutolea haja nzito, wengi ambao hawashukiwi chumvini au hawabong’oi (hawafanyi mbuzi kagoma n.k) nasikia huwa hawajali ama hawajui kabisa kuwa wana nywele huko………huruhusiwi kucheka wala kushangaa hapo!

Mwanamke, hata kama hupindi/binuka harufu itasikika, huenda wewe huisikii kwa vile umezoea lakini mpenzi wako atavuta harufu hiyo yenye utata (mchanganyiko wa jasho, ute na mavi) hivyo hakikisha huto tunywele tunaondolewa kila tunapojitokeza hata kama wewe ni mtu wa kifo cha memde tu.

No comments:

Post a Comment