Tuesday, March 24, 2009

Maji baridi na Kuzuia Mimba

Maji baridi na Kuzuia Mimba

Kuna ile imani kuwa ikiwa hutumii au hujatumia kinga dhidi ya mimba basi mara baada ya kumaliza kufanya mapenzi kimbilia bafuni na koga/oga/jiswafi na maji baridi na hivyo hutoshika mimba.

Vilevile kuna watu wanaamini kuwa ukifanya mazoezi fulani au kuru-ruka mara baada ya tendo la kufanya mapenzi bila kinga basi hutoshika mimba.

Wapo pia wanao amini kuwa ukikojoa (sio kilele) mara tu baada ya kufanya ngono bila kinga basi mimba hainasi.


Ukweli: Njia pekee ya kuepuka mimba ikiwa umefanya mapenzi bila kinga na unauhakika mpenzi kamalizia Shahawa zote ndani ni kutumia kidonge kinaitwa "after morning pill" a.k.a "emergency contraceptive" ambacho kimepewa 95% kufanya kazi ipasavyo ikiwa kitamezwa ndani ya masaa 24 toka tendo(Shahawa kuwa ndani), lakini kina weza kumezwa ndani ya masaa 72 ambayo ni sawa na siku tatu na ufanyaji wake kazi unapungua jinsi masaa yanavyopungua.


Mfano kikimezwa baada ya masaa 24 utandaji wake wa kazi utakuwa ni mdogo kiasi cha asilimia 58 na uwezekano wa mimba kutengenezeka unakuwa mkubwa.

Unatakiwa kuwa mwangalifu wakati wa kufanya mapenzi hasa kama huna mpango wa kuwa mama au baba kwa sasa, vidonge/kidonge hiki sio njia ya kudumu ya kuzuia mimba nikiwa na maana huwezi kucheza peku kila siku ukitegemea kumeza "after morning pill" inamadhara kwa afya yako.

Tumieni Condom ili mfanye kwa kujiamini zaidi.....

Makala zinazofanana


Njia za kuzuia mimba

Tumia Condom

Kutumia kondom ya wanaume

Mapenzi salama

Mimba na uzazi

Mpenzi wangu hataki kuvaa kondomu

Kutumia kondom ya wanawake

No comments:

Post a Comment