Thursday, March 26, 2009

Ngozi yako na Ngono

Ngozi yako na Ngono



Hatuwezi tukazungumzia swala la kungonoana bila kuhusisha ngozi, Ngozi laini, safi na isiyo na mabonde, mikwaruzo wala ukavu huvutia sana sio tu kwa kuiangalia bali hata kuishika na kuichezea. Miaka ya nyuma bibi zetu walikuwa wakitumia pumba za mahindi, Unga wa liwa na machicha ya nazi kusugua miili yao na pia binti/mwanamke alikuwa akipaswa kukaa ndani kwa muda fulani wakati “treatment” hiyo ikiendelea ili kuwa na ngozi nzuri, laini na yenye kuvutia kabla hujaolewa/funga ndoa.


KUWA na ngozi laini au ngozi nzuri wakati umri wako ni mkubwa (miaka arobaini na kuendelea) si rahisi kama ulivyokuwa awali hivyo unahitaji kufahamu ni vitu gani vinavyoweza kusababisha uharibifu wa ngozi (kukunjamana/ukavu) na hivyo kuchukua hatua madhubuti za kuepukana navyo. Vilevile nitakupa njia za kiasili na za kisasa za kukabiliana na hali hiyo, lakini kabla napenda nieleze yafuatayo.


Baadhi ya wanawake (hata wanaume) wanapofikia umri huu ngozi huaanza kuwa kavu, nyepesi, mistari hujitokeza sehemu ya juu ya uso (paji), kuzunguuka midomo, macho (juu na chini), vilevile ngozi hupoteza rangi yake ya awali usipo kuwa mwangalifu na kuijali ngozi yako..
Hali hiyo husababishwa na kutoondolewa haraka kwa chembechembe zilizokufa chini ya ngozi na kufanya ngozi yako kupoteza vitu vifuatavyo:-

1.hali ya kujibadilisha/kujitengeneza upya na kurudia katika hali yake ya awali ikiwa itahathirika.
2.hali ya kujikunjua ,
3.hali ya kuhifadhi maji na kusababisha ukavu na matatizo mengine ya ngozi.
4.ngozi haitaweza kudhibiti miale ya jua ijulikanayo kwa kitaalam kama “UVA” na “UVB” kwani haitakuwa na chembechembe ziitwazo “melanin” ambazo huilinda ngozi.


Yote hayo kwa kitaalamu hujulika na kama “melanocytes”, hivyo ni vyema ukafahamu kuwa jinsi umri unavyozidi kwenda ndio uwezekano wa kuwa na ngozi mbaya unaongezeka ikiwa hutoiepusha ngozi yako dhidi ya miale ya jua.


Vilevile mwanamke unapofikia umri mkubwa zaidi na kuelekea kwenye mabadiliko ya mwisho ya mwili wako ambayo husababishwa na kwenda mwisho wa hedhi au kukoma Hedhi (MENOPAUSE) ngozi yako wakati huu itahitaji matunzo maalum au ya ziada ili ibaki katika hali nzuri yenye afya na kuvutia, unapaswa kuacha kabisa vitu vifuatavyo:-


-Unywaji wa pombe ( aina yoyote ya kilevi) kwani huuwa vitamini A,B na C ambazo ni muhimu kwa afya ya ngozi.

-Epuka matumizi ya sabuni zenye au zilizotengenezwa kwa acid kwani hukausha ngozi.

-Uvutaji wa sigara ambazo hutokana na tumbaku (hii ni kemikali) huchafua damu kwa kuikosesha “oxygen” hali ambayo husababisha ngozi kujikunja .

-Usipende kutembea au kukaa juani kwa muda mrefu,wengi hupendelea kuota jua la asubuhi ambalo ndilo husababisha mikunjo kwa asilimia 80

-Epuka madawa makali ya kuchubua ngozi a.k.a Mkorogo.

-Usipende kujiweka katika wimbi la mawazo kwani hali hiyo pia husababisha uharibifu wa ngozi, jitahida kuwa na furaha ( hata kwa kujifanya) wakati wote ilimradi tu sikunje uso wako.

-Usipake vipodozi vingi na ikiwezekana paka unapohitaji na isiwe kama sehemu ya muonekano wako.

-Acha au punguza kunywa kahawa, pia usile vyakula vyenye mafuta yasio ya asili (vyakula vya kukaanga).



Vitu muhimu vya kuzingatia ktk utunzaji wa ngozi yako.


-Krimu na vifaa vyote vya urembo vilivyopo duniani havitaweza kukusaidia ikiwa wewe mwenyewe hukuijali ngozi yako tangu mwanzo lakini ulaji wa mboga-mboga, matunda na mazoezi vitakupa/kukuongezea chembechembe zote zilizokufa na kunyoosha ngozi yako kuliko krimu ya usiku ambayo ni ghali.

-Kuwa na lishe nzuri/bora (mara 3 kwa siku) na kila ukiandaa usikose kuweka mbogamboga na matunda, pia hakikisha kuwa chakula chako kina virutubisho vyote vya vitamini A, B ,C na E, vilevile iron, magnesium, potassium,zinc n.k. ambavyo mara nyingi hupatikana kwenye vyakula vikavu.

-Safisha ngozi yako mara kwa mara na vilevile isugue kwa kutumia machicha ya nazi (kwa vile yana mafuta asilia ambayo nadhani yana vitamin E na usione noma hakuna atakae kuona) unaweza hata ukaomba mwanao au mumeo akusaidie sehemu ambazo huwezi kuzifikia kama vile katikati ya mgongo n.k.

-Unaweza pia ukaongezea vyakula vyenye vitamini B1 ,2 ,6,12 ,vilevile unapaswa kunywa maji kwa wingi ili kuongeza “oxygen” kwenye damu, hulainisha ngozi, huimarisha homono .nk.

-Mazoezi ya kawaida (sio yale ya “shape up”) huimarisha ngozi kwani hufungua vijitundu vidogovidogo na kuruhusu “oxygen” kuingia kwa urahisi kwenye kila chembechembe (cell) za mwilini, kwenye “hormone” ambazo hulisha ngozi na kuongeza “OESTROGEN” ambayo husaidia kuifanya ngozi kuwa katika hali ya Ujana (kunyooka).


Ngono ni sanaa

No comments:

Post a Comment