Tumia Condom
Inaonyesha watu wengi ama ni wavivu au hawatilii maanani matumizi ya Condom. Tukizungumzia kinga bora ya magonjwa ya ngono na mimba sizizotarajiwa hii bidhaa inashika namba moja.
Condom haidhuru mtu yeyote kama zilivyo kinga nyingine za kuzuia mimba ambazo huwasababishia mateso makubwa sana wanawake na wakati mwingine kuwabadilisha kabisa kiakili na kimwili.
Sikatai kila kitu kina side effects zake, lakini jamani nani amewahi kuugua kwa sababu tu katumia Condom?
Tatizo ni kwamba baadhi yetu tunapenda kuifikiria Condom in negative way lakini kama tukiifikiria in possitive way hakika hakuta kuwa na Watoto walizaliwa "kwa bahati mbaya" na maambukizo ya UKIMWI yangepungua kama sio kuisha kabisa.
Unatakiwa kujaribu aina tofauti za Condom ili kujua ipi inakufurahisha(tamu) zaidi....n.k.
Kuna tofauti ya rangi, radha, ulaini(hizi mpya ukivaa ni kama hujavaa kitu vile), kuna za vipele, kuna nzito zaidi kwa wale wanaotoka na wadada/kaka walioathirika (lakini hawajui) au kwa mara ya kwanza(hamfahamiani vema) n.k.......so hakuna kisingizo cha kutotumia Ndomu hapo ei.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment