Tuesday, March 17, 2009

Kupenda kwa vitendo

Kupenda kwa vitendo


Kama ilivyo mambo mengine kuwa “affection” ni swala la kujifunza, baadhi ya wanaume waliokuzwa/kulia kwenye jamii yenye mfumo Dume (Waafrika kwa ujumla) huwa hawajui kuonyesha hilo hitaji, ebu tuliite “kupenda kwa vitendo” hivyo huenda sio kwamba hataki bali hajui.


Kwa maana hiyo sio mbaya ikiwa wewe mwanadada ukamfundisha nini cha kufanya, ikiwa na wewe ulikuwa hujui basi jifunzeni wote ili kuwa na uhusiano bora wenye furaha.


Nitaorodhesha mambo machache ambayo wanawake wengi huwa wanapenda kufanyiwa ili wajue kweli wanapendwa kihisia na kivitendo.

1-Hakuna kitu wanawake wanazimia kama kukumbatiwa na kupigwa busu mara kwa mara.

2-Kabla hujakurupuka kitandani hakikisha umekumbatia na kubusu hata kama kalala(hakuna raha kama kuamshwa na busu au mkumbatio).

3-Mwambie jinsi gani unampenda na unavyopenda chapati/mayai/viazi alizopika au hata jinsi alivyoandaa mlo wa asubuhi.

4-Wakati unatoka ndani kumbatia chap-chap na busu kiduchu ndio utokomee kazini, hata kama mnatoka wote kwenda kwenye kituo cha daladala unafanya hivyo kabla hujakanyaga vumbi la nje.

5-Onyesha unajali kwa kumjulia hali kwa sms au sauti mara baada ya kufika kwenye mihangaiko yako na vilevile kumbuka kufanya hivyo kabla hujaondoka eneo la shughuli zako pia hakikisha unamueleza utakuwa saa ngapi nyumbani au kama kuna mahali unapitia basi mfahamishe utakuwa huko kwa muda gani n.k.

6-Ufikapo nyumbani kumbatia na busu mdomoni sio shavuni, badala ya kukimbilia kusema yaliyojili huko utokako.

7- Mnunulie vijizawadi mara kwa mara, wazaramo hununuliwa Khanga au hereni na mikifu ya dhahabu, Wazungu hununuliwa maua, kadi au vidani vya madini tofauti, kuna wengine ukipeleka kitoweo (aina ya nyama) basi umemaliza kezi mwana mama anafurahi kweli-kweli sasa wewe fanya kile unachomudu………... sio kila siku wala kila mwezi..


8-Msaidie kusafisha mesa/jamvi mara baada ya mlo wa jioni, ikiwa umechoka hata yeye kachoka pia hivyo mkikutana nyumbani mna-share kufanya usafi ili kuokoa muda.


9-Lolote litakalo tokea kila la kheri, lakini hakikisha unabusu na kukumbatia kabla hujaanza kukoroma.

No comments:

Post a Comment