penzi ni nini hasa
Penzi halina dawa, penzi halihusiani kabisa na kufanya ngono (hivyo kubinuka aina nyingi za mibinuko haina maana ndio utapendwa au unapendwa zaidi) penzi huja kiasili huhitaji kulazimisha wala kwenda kwa Mganga....Penzi huhitaji na huchukua Muda.
Lakini je, penzi ni nini hasa?
Watu wanasema penzi halielezeki au halina tafsiri maalumu kwamba kila mtu ana maelezo yake kuhusu penzi na maelezo hayo hutegemea zaidi na uzoefu wake.
Mimi nadhani penzi ni hisia zenye nguvu ya ajabu za mtu Fulani juu ya mtu Fulani, hisia hizo hazijalishi muonekano (mavazi, sura, umbile n.k), utajiri, umri, Elimu, aina ya maisha au tabia.
Hisia hizo humfanya mtu ashindwe kufanya mambo ya kawaida ambayo huyafanya kila siku kwa vile kichwani anakuwa anamfikiria yule ampendae, hisia hizo zinaweza kupelekea mtu kubadilisha personality na tabia yake hasa pale unapofanikiwa kuwa na huyo ampendae.
Unapofanikiwa kuwa/mpata yule umpendae huwa unapata raha ya ajabu kila unapomuona, inakuwa ngumu sana kuwa mbali nae. Hisia hizo zikikomaa hukufanya uhisi maumivu yake ikiwa anaumwa, umemuudhi au kaudhiwa na mtu mwingine, anapokuwa na huzuni mpenzi wako hakika utahisi huzuni n.k.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment