Showing posts with label penzi ni nini hasa. Show all posts
Showing posts with label penzi ni nini hasa. Show all posts

Tuesday, March 31, 2009

Nenda taratibu lakini changamka katika mapenzi

Nenda taratibu lakini changamka katika mapenzi!


Mara nyingi wanawake huwa anapenda au kutaka kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na kila kitu kiende sawia kabisa bila matatizo, hii ni kutokana na sababu nyingi tofauti kama vile

-kuwa mpweke kwa muda mrefu,
-kuwa na "foleni"ndefu ya mahusiano mafupi na sasa anahisi kuwa wakati umefika wa kukaa na kutulia na mtu mmoja,
-uoga wa kuachwa/kuumizwa,
-kuhisi ameachwa(left out) kwa vile rafiki zake wana wapenzi,
-kuhisi umri umekwenda n.k.


Haijalishi una uzoefu mbaya au mzuri ktk mahusiano ya kimapenzi…unachotakiwa kufanya ni kutuliza akili na kucheza taratibu. Ukichukulia mambo taratibu itakusaidia sana kujua hisia zako juu ya mwenzio na pia kumjua/fahamu huyo mpenzi kabla mambo hayajawa “makini” hali itakayokusaidia kutoumia sana ikiwa atagundua kuwa humfai au wewe kutambua kuwa hayuko vile ulivyotegemea n.k.


Vilevile kwenda kwako taratibu kutamfanya huyo “mpenzi mpya” kuwa “comfortable” na wewe, kwa vile hautokuwa mtu wa kulazimisha mambo yatokee vile unavyotaka……..wanaume wengi hawapendi kuwa “pushed” kwa vile uhisi hawapendwi bali unapenda kufanikisha jambo fulani kama ktk maisha yako na sio kwenye maisha yenu “as a couple”.


Kumbuka kuwa wanaume hutumia uongo mwingi ili “washinde” na wakupate, hivyo kuwa mwangalifu najifunze “kuchuja” maneno/mistari yao wanapokushawishi/tongoza uwe nao, mara nyingi hutoa ahadi nyingi ambazo hu-“sound” kama wanaji-“commit” kwako kabla hata hujawajua vema.


Wewe kama mwanamke unatakiwa kuwa makini, msikivu, mwelevu na mwepesi kuhoji ikiwa utahisi unayoambiwa ni “too much….too soon”, sio macho chini na kila kitu….Ok, haya, sawa, ai wewe……ndio…..wasema kweli mjuba…..n.k.……changamka!


Kumbuka kitakacho kufanya umdondokee mtu kimapenzi kabla hata ya kungonoana sio muonekano wake tu (au pesa kwa wengine wazembe-wazembe) bali kumjua kiundani baada ya kuzungumza nae……unapomhoji mwenzio ni rahisi kujua uta-offer nini kwenye uhisiano ili uwe bora na yeye atachangia vipi ili mtoke “pea” nzuri na ya muda mrefu.


Maelezo yake kutokana na maswali yako yatakuwezesha wewe utafakari na kufanya uamuzi wa busara hali kadhalika maswali yako yatamfanya yeye afikiri zaidi ikiwa ni myeyushaji/muongo lakini “anakutaka” basi anaweza kubadili yote aliyosema/ahidi jana kwani kagundua kuwa wewe sio wa kudanganyika…..na akiendelea hamtofika mbali….hii yote nitakuwa imetokana na kuchangamka kwako kwenye kuhoji pale ulipohisi jamaa natoa ahadi kamavile ninyi ni “couple” tayari kumbe ndio kwanza mna-date.


Kumbuka mtu anapoku-“date” haina maana kuwa mko kwenye uhusiano na mara nyingi hushauriwi kufanya ngono ktk kipindi hicho……”date” inaweza kuchukua siku tatu mpaka miezi 4 kabla hujajitolea mwili wako.

penzi ni nini hasa

Misingi ya Uhusiano wa Kimapenzi

Friday, March 27, 2009

Penzi halilazimishwi

Penzi halilazimishwi!



Natambua kuwa kila mtu ana tafsiri yake ya neno mapenzi au maana halisi ya kupenda. Moyo wako siku zote unajua pale unapompenda mtu na hivyo huhitaji kuulazimisha, kuushawishi au kuomba ushauri kwa watu wengine kama itakuwa sahihi kuwa na fulani au la!

Penzi na jinsi linavyojitokeza ni hadithi ndefu na inachanganya, sote tunajua swala zima la mapenzi linachanganya na halina kanuni lakini ni moyo wako pekee ndio utakao jua kama hapo "umefika bei" au la!


*Penzi tamu na mara nyingi hudumu kwa muda mrefu ni lile lililo na chanzo kwenye urafiki. Urafiki mwema siku zote huwa hauna mwisho hali kadhalika mapenzi ya kweli hayana mwisho sasa hebu changanga pamoja uone matokeo.

Mnapokuwa marafiki kwanza nakuzoeana sana kiasi kwamba mnasaidiana vilevile mnakuwa huru au wazi ktk kuzungumzia mambo binafsi kama vile furaha, matatizo,mafanikio namengine mengi muhimu napengine kujua mapungufu yenu ambayo kama marafiki mnakuwa tayari mnajua jinsi ya kuishi nayo aukuyavumilia na hivyo mnaendelea na maisha yenu yenye furaha na amani kama marafiki na wakato huohuo wapenzi.


Tatizo la penzi lililojengeka ktk urafiki ni kwa mmoja wenu kuhofia urafiki kufa ikiwa ataziweka hisia zake wazi kwa mwenzie. Ikiwa utamkataa ni wazi kuwa itakuwa ngumu sana kwake kuvumilia kukuona wewe kuwa na mtu mwingine kama mpenzi na sio yeye.


*Penzi liloegemea kwenye kupendeza/kuvutia hufa au hufikia kikomo mara tu mmoja wenu anapobadilika au kutovutia tena kutokana na sababu tofauti za kimaisha. Ukitaka penzi libaki pale pale basi ni wajibu wako kuendelea kuwa hivyo ulivyo (kupendeza/kuvutia).


Nakumbuka juzi nikiwa kwenye “office” , Jamaa (nafanya nae kazi) akinilalamikia kuwa “My wife didn’t look like that when we met, she was so hot like those women” (akionyesha wanawake wenye maumbile mazuri na wamependeza kimavazi)” nikamuangaliaaaaa kisha nikamuuliza unadhani hakuvutii tena?


Akasema “ndio, hata kufanya mapenzi inakuwa ngumu siku hizi”. Nikamuuliza tena huoni kuwa amekuwa hivyo alivyo kwa sababu yako? Akauliza “kwanini” nikamwambia hukumwambia wazi kuwa unachopenda kwake ni “the way she look, nothing more” angejua angefanya uamuzi wa busara kuliko kufunga ndoa na wewe na kisha kukuzaliya watoto. Nikamwambia the woman needed/needs ur love and support!........

Penzi lisilo na mwisho ni lile linalijotokeza kiasilia (naturally) kwamba unakutana na mtu (sizungumzii love at 1st sight hapa) kisha mnajikuta mnapendana kwa dhati penzi hili hunawiri vizuri sana na hudumu kwa muda mrefu na ikitokea mmoja kumuacha mwenzie basi itakuwa ni sababu “nzito” ambayo ni kifo (ndio pekee kitatenganisha penzi hili).


Atakae baki humuia vigumu sana kuwa na mpenzi mwingine na itamchukua muda mrefu sana “kumdondokea” mtu mwingine “Bond” ya penzi hili ndio wengine huita penzi la kweli.


penzi ni nini hasa

Misingi ya Uhusiano wa Kimapenzi

Tuesday, March 17, 2009

penzi ni nini hasa

penzi ni nini hasa


Penzi halina dawa, penzi halihusiani kabisa na kufanya ngono (hivyo kubinuka aina nyingi za mibinuko haina maana ndio utapendwa au unapendwa zaidi) penzi huja kiasili huhitaji kulazimisha wala kwenda kwa Mganga....Penzi huhitaji na huchukua Muda.

Lakini je, penzi ni nini hasa?

Watu wanasema penzi halielezeki au halina tafsiri maalumu kwamba kila mtu ana maelezo yake kuhusu penzi na maelezo hayo hutegemea zaidi na uzoefu wake.

Mimi nadhani penzi ni hisia zenye nguvu ya ajabu za mtu Fulani juu ya mtu Fulani, hisia hizo hazijalishi muonekano (mavazi, sura, umbile n.k), utajiri, umri, Elimu, aina ya maisha au tabia.

Hisia hizo humfanya mtu ashindwe kufanya mambo ya kawaida ambayo huyafanya kila siku kwa vile kichwani anakuwa anamfikiria yule ampendae, hisia hizo zinaweza kupelekea mtu kubadilisha personality na tabia yake hasa pale unapofanikiwa kuwa na huyo ampendae.

Unapofanikiwa kuwa/mpata yule umpendae huwa unapata raha ya ajabu kila unapomuona, inakuwa ngumu sana kuwa mbali nae. Hisia hizo zikikomaa hukufanya uhisi maumivu yake ikiwa anaumwa, umemuudhi au kaudhiwa na mtu mwingine, anapokuwa na huzuni mpenzi wako hakika utahisi huzuni n.k.