Tuesday, March 24, 2009

Usafi na Ngono

Usafi na Ngono


KILA mmoja wetu anafahamu nini maana ya usafi, lakini baadhi ya watu wamekuwa hawatilii maanani, hawana habari, hawajali pia wapo wengine hawajui kabisa waanzie wapi kuwa wasafi.

Mapenzi yanahusisha mambo na maungo mbalimbali kama vile miguu (legs), miguu ya kukanyagia (feet) na kucha zake, mikono, viganja ikiwa ni pamoja na kucha zake,macho, pua, midomo ya nje (lips), kinywa, nyayo, makalio, alafu ndio zinafuata sehemu nyeti.

Maungo hayo yote yana maana na umuhimu wake katika swala zima la mapenzi hasa yakitumiwa ipasavyo na yakiwekwa katika hali ya usafi, vinginevyo utampoteza mpenzi wako au kuharibu uhusiano wenu mzuri mlionao.

Usafi ninaouzungumzia hapa sio ule wa kuoga na kupaka Manukato (perfum)/Lotion/mafuta, kufua/kunyoosha nguo pekee bali ni usafi ule wa ndani ambao baadhi ya wanawake hufundishwa tangu wakiwa na umri mdogo.

Hali kadhalika wanaume pia hufundishwa jinsi ya kujisafi baadhi ya maeneo ya miili yao, lakini inasikitisha kuwa wanaume wengi hawajali kabisa usafi uwe ni ule wa kawaida au ule wa kunako nyeti.

Wapo baadhi ya wanume na wanawake ambao hupenda sana kulambwa lambwa katika maeneo Fulani ya miili yao wakidai kuwa ndio inayowaongezea nyege, lakini cha kusikitisha ni kuwa watu hawa hawajali/hawatunzi maeneo hayo na badala yake kutegemea mwanamke amshughulikie.

Utunzaji wa kinywa


Kunatofauti kati ya kusafishakinywa kama sehemu ya usafi wa mwili wako na ule usafi wa kinywa kwa ajili ya kuvutia au ku-share kinywa hicho na mtu mwingine a.k.a Mpenzi.

Japokuwa wengi tunajitahidi kuisafisha midomo/vinywa vyetu bado tuna sahau maeneo muhimu kama vile sehemu ya juu ya kinywa ambako huko hujikusanya uterezi ambao hupelekea mtu kuwa na nyuzi nyuzi wakati anaongea, kucheka, kuimba n.k.

Vilevile ikumbukwe kuwa ukisafisha meno vizuri nakuacha ulimi utakuwa umeondoa harufu ya kinywa chako kwa kiasi kidogo sana, utakapo m-busu mtu kwa kutumia ulimi/mate bado utakuwa unatoa harufu, hutoisikia wakati unabusu kutokana na raha bali baada ya busu mwenzako atajua domo lako lanuka….aibu sio?

Midomo ya nje (lips) wanawake wengi huwa wanakimbilia kuipaka mafuta/lipbum/lipstick n.k. bila kujali usafi wa midomo hiyo ya nje. Midomo hii ya kubusia nayo husuguliwa na mswaki ili kuondoa uchafu unaosababishwa na mate ambayo husababisha ukavu ambao unaweza kupelekea midomo yako kupasuka au kutoa harufu mbaya midomo hunuka kutokana na mate.

Sasa unachotakiwa kufanya ni kuisugua taratibu kwa kutumia mswaki wako ambao utakuwa hauna dawa na utakuwa msafi(mara baada ya kusafisha meno) kwa kufanya hivyo kutaifanya midomo yako ya nje iwe laini wakati wa kuifanyia kazi iwe ni kubusu au kunyonya.

*Sugua meno yako kila siku asubuhi na jioni, ikiwezekana kila baada ya kula chakula. Anza kwa kusugua meno pande zote juu, chini, katikati na pembeni

*Safisha mswaki wako na usugue ulimi wako sehemu ya katikati na pembeni rudia mpaka ukitema mate yasiwe na mrendamrenda, kisha suuza na maji ya vuguvugu.

*Ikiwa “unaasili” ya kuwa na nyuzinyuzi katika kinywa yaani ukiongea/kucheka/ kupiga miayo n.k kunatokea mate yaliyoungana mithili ya uzi, hali hiyo hakika hutia kichefuchefu.

Unachotakiwa kufanya kila baada ya kula ni kutafuna kipande cha limau/ndimu/mbilimbi/mdalasini ambayo itasaidia kukata mate au tafuna bazoka zenye MINT ambazo hazijaongezewa sukari ili kuepusha harufu mbaya ya kinywa na meno yako yasioze.

NYWELE-zinatambulisha utanashati/urembo wa mtu (personality), uhai/utu alionao (vitality), jinsia aliyonayo (sexuality) vilevile zina nguvu ya ajabu katika swala zima la mapenzi.

Nasikia kuna utamaduni wa watu Fulani ambao huunganisha nywele za Bibi harusi/ndoa na Bwana harusi/ndoa kwa kuzisuka siku hiyo ya harusi/ndoa kama ishara ya kuwa pamoja katika maisha yao yote ya ndoa.

NYWELE ZA MWANAMKE.

Nywele za kichwani za mwanamke(haijalishi kama ni asilia au za bandia ilimradi ziko kichwani) ni sehemu ya kivutio/urembo wake ikiwa zitajaliwa na kupewa matuzo yanayotakiwa ikiwa ni pamoja na kuzisafisha. Nywele za mwanamke kwa baadhi ya wanaume zinaamsha nyege ikiwa zitalowa chapachapa wakati wa mvua.

Nywele hizo huwa kivutio zaidi ikiwa zitavurugika na kulowa jasho wakati mnaendelea kufanya mapenzi kuliko zikibaki katika style ileile uliyotengeneza asubuhi.Kwa hivyo mwanamke usihamishie akili kwenye mtindo wako wa nywele na badala yake hamishia akili kwenye tendo lenyewe ambalo ni ngono.

Nywele za mwanamke ziotazo Kwapani, miguuni, kidevuni, kifuani ni lazima(well ni vema) ziondolewe kila baada ya wiki au wiki tatu inategemea umetumia njia gani kuziondoa bidhaa za kisasa, asali, sukari wembe n.k. unatakiwa kuwa laini sehemu hizo wakati wote.

KUNAKO NYETI- unatakiwa kupunguza kidogo(usiondoe zote unless mpenzi wako anapenda kipara) sehemu ya juu hadi mwanzo wa kisimi kisha ondoa nywele zote za pembeni, kwenye mashavu mpaka kule karibu na sehemu ya nyuma.

Tafadhali unapoondoa nywele sehemu hizo usitumie aina yoyote ya madawa ya kisasa ili kuepuka matatizo ya kiafya na badala yake tumia wembe na chukua muda wa kutosha kuondoa nywele sehemu hizo.

No comments:

Post a Comment