Thursday, March 26, 2009

Jinsi ya Kuwa Sexy

Jinsi ya Kuwa Sexy!

Sina hakika neno “sexy” kwa kiswahili ni nini hasa, je ni kuvutia in a sensual way kwamba watu wanakuona uko kingono-ngono (picha wanaipata wanapokuona ni unavyokuwa juu ya vitanda vyao)?


Huhitaji kuwa mzuri wa asili, mrembo, mwenye umbo zuri au Tajiri ili kuwa “sexy”, huitaji kwenda na wakati ktk uvaaji wako, huitaji kuwa mnene au mwembamba ili uwe “sexy” bali ni jinsi hivyo ulivyo, jitihada zako za kuwa ulivyo hasa kwa kufanya vile vitu unavyopenda kuvifanya bila kuhofia wengine watakufikiriaje na bila kusahau swala zima la kujiamini wewe kama wewe.


Baadhi ya watu huchanganya swala la kujiamni na badala yake wanakuwa na viburi mbele za watu wakidhani kuwa huko ndio kuwa- “sexy”.



Pia kumbuka kuwa kuna vitu vingine tunavifanya kila siku lakini kwa watu wengine wanaviona ni “sexy” kama vile

-sauti,
-jinsi unavyoongea na kulamba midomo yako,
-jinsi unavyoona aibu kujieleza,
- miondoko yako,
-unavyotazama,
-unavyotafuna,
-unapokuwa jikoni unasonga ugali n.k.


U “sexy” hutegemeana na mtu mwenyewe anaona kama ilivyo uzuri……kwamba uzuri uko machoni mwa mtazamaji.


Wakati mwingine kuwa “sexy” ni hisia zako mweyewe kwamba unahisi kuwa uko hivyo kutokana na ulivyo vaa siku hiyo au kwa vile umenenepa au umepunguza uzito….
Lakini huwezi kukurupuka tu ukaanza kujihisi kuwa uko “sexy” unahitaji kufanya jitihada fulani sio.

Mwanamke

1-Kuwa safi na nukia vizuri, sasa basi kuoga mara tatu kwa siku ni muhimu ili kufanya ngozi yako ipendeze na kuboreka kutokana kufungua vijitundu vya kupitisha hewa.
Kunikia ninakokuzungumzia sio lazima kuwe kwa manukato ghali unaweza ukawekeza kwenye “vikausha kwapa” (deodorant) nakisha ukamalizia na mafuta yako ya “Rays”) well tumia aina yoyote ya mafuta/lotion inayopata na aina ya ngozi yako na ambayo haitochukua/badilisha harufu yako asilia ya mwili.


2-Hakikisha unaondoa nywele zisizotakiwa au zile ambazo hupendi kuziona, yaani zinakuogofya kama vile kwapani, kwenye mstari wa ikweta, sehemu ya tumboni/kifuani (mwanamke huitaji nywele sehemu hizo), miguuni, mikononi, kwenye vifundo vya vidole miguuni, yetini, kidevuni na mustachi (kama unazo sehemu hizo zifanyie utaratibu tafadhali....utakuwa kama baba).


3-Vaa vizuri na jitahidi kuwa na mtindo wako mmoja wa uvaaji na pia jaribu kuwa mbunifu na ulijue umbile lako…..kwamba vaa kutokana na umbile lako ili kuepuka vazi kukuvaa wewe Mfano:



Kila vazi unalovaa lazima liwe na rangi inafanana na kidani cha mkufu wako, rangi za mavazi yako ni zile zilizopoa tu au kila kiatu unachovaa lazima kiwe na kisigino kirefu (nadhani umenielewa nina maana gani), hali hiyo itakufanya ujiamini zaidi ktk uvaaji wako, vilevile siku ukibadilisha na kuvaa tofauti na mtindo wako unaweza ukahisi kuwa uko-Sexy…….ukipata hisia hiyo utajiamini na wengine watakuona vile unavyohisi kwa ndani.


Ukishindwa kabisa basi wewe wekeza kwenye Jeans…..wanasema Jeans ni “ultimate sexy accessory” chagua ile itakayo shikilia vema makalio yako na kuchonga vema umbile lako…hahaha.



Hakikisha hutolei macho sana “trends” kama skinny jeans au hipster badala yake wekeza kwenye ubora na wakati huohuo usisahau kuwa lazima iwe “classic” kwamba utaweza kuvaa vazi hilo kwa miaka mingine 5 ijayo bila kuhisi umepitwa na wakati.


4-Jifunze sanaa ya urembo, sio lazima ukandike poda na mirangi ya ajabu ajabu bali unaweza ukawa unatumia “foundation” kwenye T-zone zako kisha ukaongeza uwanja na lipgloss au mafuta ya “Rays” ili midomo yako isikaukiane, hakikisha unatengeneza nyusi zako kufuatana na uwingi wake au ukubwa wa macho yako....

5-Hakikisha kila kona ya mwili wako inatoa pumzi nzuri (isipokuwa pale utakapo ponyokwa na ushuzi ofcoz). Hakikisha ukicheka/ongea/nong’oneza, tabasamu harufu inayotoka hapo ni safi na inaita hivyo ni vema kabisa ikiwa utasafisha kinywa chako hasa ulimu (ulimi ndio kianzilishi cha harufu mbaya ya mdomo na sio meno)……jaribu kusugua ulimi alafu acha meno kisha mpumulie mtu usikie atakwambiaje?


6-Jifunze kuwekeza kwenye nguo za ndani, jitahidi kuwa na chupi/sidiria/gagulo nzuri na zenye ubora…..kumbuka matiti yakiwekwa vizuri kwenye sidiria utakachokiweka juu pia kitakaa vema, hali kadhalika chupi ukikosea rangi au aina basi unakuwa umeharibu kila kitu.


7-Hakikisha unafanyia kazi yale maeneo ambayo unadhani yanakufanya uwe noma/ovyo kuyaonyesha mbele ya mpenzi wako hali inayofanya mfanye mapenzi mkiwa mmejifunika au gizani.


Unaweza kufanikiwa kwa kufanya mazoezi au kwa sababu zozote unadhani huwezi basi tafuta aina ya viwalo ambavyo vijana kwa wazee wengi siku hizi wanaviona kuwa ni “sexy” kama ilivyo shanga ikiwa wapenzi wao watavitinga kwa kufanya hivyo kutafanya mpenzi wako aone vizuri umbile lako, alizoee na kulipenda vile lilivyo.

Usafi wa Matako na Uke

Jinsi ya kusafisha Uke wako

Kuma Yangu Inanuka

Ngono ni sanaa

No comments:

Post a Comment