Ni nini kinachotokea kwa wasichana?
Je niko sawa? Mambo ambayo huwatia wasiwasi wanawake. Kila mtu ana umbile lake na ukubwa, lakini wengine wetu huwa na wasi wasi, hasa kuhusu viungo vyetu vya uzazi. Hiyo ni kawaida lakini ubaya ni kuwa wakati mwingi watu huona haya kuzungumza chochote kuhusu swala hilo hasa likifungamanishwa na ngono. Kwa kurahisha mambo basi hapa tuna maswali na majibu kwa maswala yanayohusu viungo vyetu vya uzazi ambayo mara nyingi hutatanisha. Tunatumai yatakwondolea hofu na kukutuliza. Kinachowatia wasiwasi zaidi wanawake 1. Moja ya matiti yangu ni kubwa zaidi ya lingine. Je hili ni jambo la kunitia wasiwasi na naweza kufanya nini kuhusu swala hili? Labda lingekuwa jambo la kutia wasi wasi zaidi kama matiti yako yote mawili yangekuwa sawa sawa kabisa. Utaratibu unaotokea wa jinsi tunavyokua na kuimarika kuanzia utotoni hadi kubaleghe, ukitazama miili yetu , japo upande wa kulia unafanana na wa kushoto huwa haiko sawasawa kabisa. Hivyo basi si wewe pekoe, wanawake wengi wana matiti yenye umbo na ukubwa usiofanana. Ingawa hivyo si jambo linalogundulika kwa urahisi na mtu mwengine… Lakini wanawake wengine wanaohisi tofauti sana, huongezea kitu kama pamba hivi wanapovaa sidira ili kusawazisha. 2. Chuchu za matiti yangu zaonekana kupinda, nifanyeje? Chuchu zinazoonekana kupinda si kasoro, na wanawake wengi wako hivyo. Wakati mwingine mwili wa mwanamke unapokua chuchu za matiti huchomokea nje. Inaeleweka kwamba matiti ni kiungo muhimu kwa mwanamke, na hata yakiwa chuchu moja au zote mbili zimechomokea upande tofauti , si hoja bado anaweza kufurahikia mapenzi, na pia tutekeleza kazi zote za uzazi zinazotekelezwa na kiungo hicho, ikiwemo kunyonyesha wakati mwanamke akipata mtoto. Ila tu ni vyema kuhakikisha unakuwa mwangalifu na kwa kuona kwamba chuchu ni safi, kwani huwa rahisi kuambukizwa viini vya magonjwa kama maji maji au maziwa kwa akina mama wanaonyonyesha yanabakia kwenye mikunjo. 3. Ni kiungo gani hiki kilichochomoza nje kidogo ya uke wangu? Hicho kinaitwa kinembe au kisimi kwa Kiswahili , kwa kiengereza kinaitwa clitoris. Ni mojawapo ya kiungo muhimu kinachounda ‘kuma’ ya mwanamke na kinachosisimua hisia za kimapenzi kwa hali ya juu kinapopapaswa. Wakati mwanamke anapopata ashiki au uchu wa mapenzi, kuguswa guswa kwa kisimi kwaweza kupandisha starehe ya mapenzi na kumfanya mwanamke kufikia kilele cha starehe hizo kwa haraka. 4. Na je kile kiitwacho cervix kwa kiingereza nacho ni kipi? Ndani kabisa ya uke kuna shingo la mfuko wa uzazi, hii ndio njia ya kuelekea kwenye nyumba ya uzazi. Wakati wa kufanya ngono manii ya mwanamme hupitia njia hii na mbegu ya wanamme ikikutana na yai la mwanamke mimba hutungwa. Wanawake wanaotumia vifaa vya vizibo maalum vya kuzuia mimba kama vile diaphragm au caps, vifaa hivyo hupachikwa katika kilango hicho cha kuingia katika nyumba ya uzazi, hivyo basi manii kushindwa kuingia. Vifaa hivyo pia huandamana na dawa zinazoua mbegu hizo ili kuzuia uwezekano wowote wa mbegu ilopenya kukutana na yai la mwanamke. 5. Na mbona mashavu ya uke wangu ya upande wa kushoto yanatofautiana kwa ukubwa na yale ya upande wa kulia? Kama tulivyosema hapo awali, viungo vyetu vya mwili vya upande wa kulia ingawa vinafanana na vya upande wa kushoto kawaida havifanani kabisa kabisa. Huwa kunatofauti kidogo – hivyo kwa mashavu ya ukeni ni vivyo hivyo. Uke una aina mbili za mashavu, mashavu ya ndani na mashavu ya nje. Mashavu ya ndani ambayo huwa ni madogo ni ya rangi ya pinki. Mashavu ya nje kwa kawaida yanaweza kuwa makubwa marefu na yenye ukubwa usiolingana. Huwa na maumbile na ukubwa tofauti, na huwa makubwa zaidi na manene wakati mwanamke anapopata ashiki ya mapenzi. 6. Hedhi yangu haiji kwa majira sawa – hii ni kwa nini? Kutokuja kwa hedhi kwa majira yanayolingana ni jambo la kawaida kwa msichana anapoanza kupata hedhi, na hali hiyo inaweza kuendelea kwa hadi miaka miwili kabla mfumo maalum wa mambo kujistawisha. Hata hivyo wanawake wengine huwa na mabadiliko katika utaratibu wao wa hedhi hata wanapokuwa watu wazima. 7. Mie napata hedhi yangu kwa siku mbili/tatu, tu je hili jambo la kutia wasiwasi? Siku za hedhi kwa kawaida huwa ni kwa siku tatu hadi saba. Kama tulivyosema, huchukua mda kabla mwili wa mwanamke kupata utaratibu maalum wa hedhi, na wanawake wengine hupata dhiki kuutambua utaratibu kamili wa hedhi zao. Pia maswala mengine kama vile kuwa na dhiki (stress) yaani wasiwasi, yanaweza kutatiza majira ya mayai kutoka na hivyo basi kuvuruga ratba ya hedhi. |
Wednesday, March 11, 2009
Wasichana na kubalehe
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment