Tuesday, March 24, 2009

Shahawa zinaniwasha

Shahawa zinaniwasha....


Jibu:Kwa kawaida Shahawa haziwashi au hata kusababisha muwasho unless hupatani nazo yaani uwe na aleji(Allergy to Semen/Sperm), kitu nitakachoweza kuhisi kuhusiana na tatizo lako ni maambukizo ya Fangazi/si au wengine huiita “Yeast” kitaalamu inajulikana kama “Candida Albicans” ambapo ule ukakasi/uchachu (unategemea na lishe ya mpenzi wako) unapoingia kwenye vijipasuka/vipele vilivyopasuka kwa ndani husababisha muwasho.
Nakushauri unamuone Daktari ili akupime (atahitaji mkojo au swab ya majimaji huko ukeni) kisha atakushauri na kukupa matibabu kutegemeana na tatizo alilotambua kwenye vipimo vyake.

Afya ya uke ni muhimu sana kuliko hata kinywa au uso wako na unatakiwa mwangalifu wakati unatumia sabuni, maji (chemsha ili kuwa na uhakika), vifaa unavyotumia kujisafishia ukiwa Gym au kama unaishai nyumba za kupanga zenye Kopo/bomba moja chooni, choo kwani kuna vyoo vimejaa kiasi kwamba ukichutama sehemu zako nyeti zinatishia kugusa vinyesi vya watu wengine, taulo la kujifutia na hata uchangiaji wa nguo za ndani (hata kama unafua kwa Jick) still unakuwa kwenye hatari ya kuambukizwa bila kujijua.


Ninachojaribu kusema hapa ni kuwa usijisikie vibaya kwenda kumuona Daktari Bingwa wa Magonjwa ya kike kwa ushauri wa kitibabu hali kadhalika dawa, kwani dawa zinapatikana kwa wingi na nyingine zinaozea stoo kwa vile wanawake wanaona aibu kwenda kuomba ushauri ili kupata matibabu.

Magonjwa ya ngono kwa wanawake ukiachilia yale makuu kama kisonono, kaswende, HIV n.k. yapo mengine madogo madogo ambayo sio lazima uyapate kwa kufanya ngono bali kwa njia nyingine zitokananzo na mitindo ya maisha tunayoishi, kutokujua/kutokujali afya ya uke, mabadiliko ya homono hasa kama wewe ni mtumiaji wa madawa ya kuzuia mimba n.k.

No comments:

Post a Comment