| Kondom ya wanawake |
Mimi ni msichana, mimi ni mwanamke nieleze jinsi ya kutumia kondom ya wanawake? - Hakikisha umeangalia mda wa matumizi wa kondom uliyonayo. Kama mda wake (expiry date) wa matumizi umekwisha basi haikufai. Fungua kipakiti chenye kondomu wakati tu ukiwa tayari kuitumia. Kuwa makini usiipasue kuioboa au kuiharibu. Kwa makini itoe kondomu kutoka kwenye pakiti yake. Ikihitajika ongeza kilainishi (lubricant) zaidi katika viringi laini maalum vilivyotumiwa kutengezea kondom ya kike. (Kwa kawaida kondom ya wanawake huuandamana na kilainishi (lubricant) chake ili kurahisisha uvaaji.)
- Kuivaa kondom hii kwa urahisi, chuchumaa, huku ukitanua magoti, au simama huku mguu mmoja ukiwa umekanyaga meza ndogo, au kiti kisicho kirefu. Ichukue kondom, huku kilango chake kikiwa kinaning’inia kuangalia chini. Kibofye kiringi cha ndani (sehemu iliyofungwa ya kondomu) kwa kutumia kidole gumba na kidole cha kati.
- Sasa weka kidole cha shahada katikati ya kidole gumba na kidole cha kati. Katika jinsi hii, huku ukiendelea kubofya kiringi cha ndani cha kondom hadi kiwe mfano wa nambari nane, na huku ukiwa umechuchumaa na kutanua magoti, tumia mkono wako mwingine kutanua mashavu ya uke wako na uiingize ukeni kondom hiyo taratibu ukianza na hicho kiringi cha sehemu iliyofungwa ya kondom.
- Ukisha kuiingiza kidogo ukeni sasa tumia vidole vyako vya shahada na cha kati kusukuma ndani sehemu iliyobaki ya kondom huku ukitanua tanua kwa ndani ili isijikunje. Kile kiringi kilichoko sehemu ya wazi ya kondom, kitabaki nje ya uke. Kondom ya kike inaweza kuvalia masaa manane kabla ya kufanya ngono.
- Lakini wakati wa kufanya mapenzi hakikisha kwamba kondom hiyo iko mahala pake vyema wala haijakunjika. Kama imekunjika basi itoe na ongeza tone la kilainishi kisha uipachike tena.
- Ni vyema kujua kwamba kwa sababu karibu nnchi moja ya kondomu itabaki nje ya uke, wakati wa kufanya tedno la ndoa, itakuwa rahisi kumwelekeza mpenzio pale atapouingiza uume wake ukeni. Kwa sababu akikosea na kuingiza kando nje ya kondom haitafanya kazi na huenda ikaleta madhara. Kosa hilo likifanyika, bora mpenzio atoke kwanza nawe uitoe kondom hiyo na uvae nyengine. Kondom ya kike inahitaji uzoefu ili kutumika vyema bila usumbufu.
- Wakati mpenzi wako atakapotoa shahawa na kutoka, ibane na uisokote kondomu katika sehemu ya kiringi cha nje, ili manii yabaki ndani . Ivute polepole na kiringi cha ndani kitajibofya na kutoka nje.
- Ni vyema kutumia kondom mpya ya kike kila mara unapofanya mapenzi.
- Wanawake wengi hutatanishwa na jinsi ya kutumia kondom hii, hivyo basi ni vyema kutembelea klininki ya mpango wa uzazi iliyo karibu nawe au kliniki ya vijana ili kupata maelezo zaidi na usaidizi kutoka kwa wataalamu wa maswala ya afya ya uzazi kama vile daktari wako au nesi.
|
No comments:
Post a Comment