Showing posts with label mimba. Show all posts
Showing posts with label mimba. Show all posts

Sunday, March 18, 2012

Upungufu wa Damu Kipindi cha Ujauzito


Upungufu wa damu (anaemia) hutafsiriwa kama kupungua kwa kiwango cha hemoglobin katika damu damu chini ya kiwango kinachokubalika kiafya. Kiwango cha kawaida cha haemoglobin (Hb) katika mwili wa binadamu ni kati ya gramu 12 mpaka 14 kwa kila mililita ya damu. Hata hivyo shirika la afya duniani (WHO) linatambua kiwango cha mpaka 11gm/mililita kuwa cha kawaida kwa mama mjamzito. Hivyo basi mjamzito mwenye kiwango chochote cha haemoglobin chini ya 11 gm/mililita hutafsiriwa kuwa na upungufu wa damu. Hata hivyo nchi nyingi hasa zinazoendelea hutambua kiwango cha mpaka gramu 10 kwa mililita kuwa ni upungufu wa damu kwa mjamzito.

Kwa mjamzito anayehudhuria kliniki kwa mara ya kwanza, upungufu wa damu kipindi cha ujauzito humaanisha kiwango cha hemoglobin chini ya <11.0 g/dL, na mimba inapofikisha wiki 28 upungufu wa damu hutambuliwa iwapo hemoglobin itashuka na kuwa chini ya 10.5 g/dL.
Kwa kuzingatia hilo, mama mjamzito hushauriwa kupima wingi wa damu siku anapohudhuria kliniki kwa mara ya kwanza na pindi mimba inapofikisha wiki 28.

Viwango vya Anaemia
Upungufu wa damu unaweza kugawanywa katika viwango vikuu vinne, yaani upungufu wa damu wa kawaida (mild anaemia) ambao ni kati ya 9-11 gm/ml, upungufu wa damu wa kati (moderate anaemia) ambao ni kati ya 7-9 gm/ml, upungufu wa damu mkali (severe anaemia) ambao ni kati ya 4-7 gm/ml na upungufu wa damu mkali zaidi (very severe anaemia) ambao ni chini ya 4gm/ml.

Mzunguko wa madini ya chuma mwilini
Kwa kawaida mwili wa mwanamke huifadhi gramu 3.5 mpaka 4.5 za madini ya chuma. Asilimia 75 huifadhiwa kama hemoglobin katika chembe damu nyekundu, asilimia 20 kama ferritin katika mifupa na asilimia 5 inayobaki huifadhiwa katika misuli na vimeng’enyo vingine vya mwili.
Wanawake wasio wajawazito hupoteza karibu gramu 1 za madini ya chuma kutoka katika seli za mwili zinazokufa kila siku na gramu 1 zaidi kila siku wanayokuwa kwenye hedhi.

Ukubwa wa tatizo
Upungufu wa damu kipindi cha ujauzito ni tatizo linalowakumba kina mama wajawazito wengi sana, siyo tu Tanzania bali nchi nyingi zinazoendelea. Inakisikiwa kuwa karibu theluthi moja ya wajawazito katika miezi mitatu ya mwisho ya ujauzito hukumbwa na tatizo hili.
Kwa mujibu wa WHO, inakadiriwa kuwa karibu asilimia 56 ya wajawazito huko kusini mashariki ya Asia hukumbwa na tatizo hili. Kwa hapa Tanzania, hakuna takwimu sahihi kuhusu tatizo hili. Sehemu nyingine duniani, inakadiriwa kuwa karibu asilimia 4-16 ya vifo vinavyotokana na ujauzito husababishwa na upungufu wa damu. Aidha upungufu wa damu wakati wa ujauzito huongeza uwezekano wa madhara kwa mtoto ikiwemo kifo.

Chanzo cha upungufu wa damu wakati wa ujauzito
Kipindi cha ujauzito huambatana na mabadiliko mbalimbali ya mwili. Moja ya mabadiliko hayo ni ongezeko la maji (plasma volume) katika mzunguko wa damu. Katika hali hii, pamoja na kwamba kiasi cha damu huonekana kuongezeka, kiwango cha hemoglobini hupungua mpaka kufikia 11.5mg/dl.
Karibu asilimia 85 ya anaemia wakati wa ujauzito husababishwa na upungufu wa madini ya chuma mwilini. Upungufu wa madini ya chuma unaweza kusababishwa na kula chakula chenye kiasi kidogo cha madini haya au mwili wa mjamzito kushindwa kutunza madini ya chuma ya kutosha kutokana na ama mimba zilizopita au kupoteza kiasi kingi wakati wa hedhi kabla ya kushika mimba.

Vyanzo vingine ni pamoja na
  • Upungufu wa folic acid
  • Ugonjwa wa sickle cell
  • Lishe duni kabla na wakati wa ujauzito
  • Kupoteza damu kwa sababu ya kuumia au kuwa na minyoo (hookworms)
  • Ugonjwa wa malaria wakati wa ujauzito
  • Ugonjwa wa chembe damu nyekundu ujulikanao kama beta thalassaemia. Ugonjwa huu huwapata zaidi watu wanaoishi Asia ya kusini, Ulaya ya kusini na Afrika.
  • Upungufu wa vitamin B12
  • Ugonjwa sugu wa kuvunjika chembe damu nyekundu (chronic haemolysis) kama vile ugonjwa kurithi wa chembe damu nyekundu (hereditary spherocytosis)
  • Ugonjwa wa kupoteza hemoglobin kupitia mkojo (paroxysmal nocturnal hemoglobinuria)
  • Saratani ya damu (leukemia)
  • Matatizo ya kupoteza damu kwenye njia ya chakula (gastrointestinal bleeding)
  • Matatizo katika utumbo hasa wakati wa ujauzito.
Vihatarishi vya tatizo hili
  • Masuala ya kijamii kama vile umri wa mjamzito, kiwango chake cha elimu na uelewa kuhusu afya yake, kama ana mwenza wa kumsaidia kiuchumi, makazi anayoishi vinaweza kuchangia mjamzito kupata upungufu wa damu
  • Vihatarishi vingine ni vile vinavyohusu masuala ya uzazi kama vile idadi ya mimba zilizotanguli (waliowahi kuzaa wana hatari ya kupata anaemia kuliko wanaopata mimba kwa mara ya kwanza), kuwa na mimba ya mapacha na kuwa na historia ya kuzaa mtoto njiti
  • Vihatarishi vingine vinahusu tabia za mjamzito kama vile uvutaji sigara, unywaji wa pombe na kutohudhuria kliniki wakati wa ujauzito
  • Pia kuwa na magonjwa kama vile kisukari, magonjwa ya figo, pamoja na shinikizo sugu la damu
Madhara ya upungufu wa damu kwa mama na mtoto
Sehemu nyingine duniani, inakadiriwa kuwa karibu asilimia 4-16 ya vifo vinavyotokana na ujauzito husababishwa na upungufu wa damu. Aidha upungufu wa damu wakati wa ujauzito huongeza uwezekano wa madhara kwa mama na mtoto ikiwemo kifo. Madhara haya ni pamoja na
  • Madhara kwa mama kipindi cha ujauzito: kukonda au kuongezeka uzito kwa kiasi kidogo sana, kuhisi uchungu kabla ya muda, kondo la nyuma kutunga pasipostahili, shinikizo la damu wakati wa ujauzito, na chupa kupasuka kabla ya wakati.
  • Madhara kwa mama wakati wa kujifungua: kupatwa na uchungu usioeleweka na usio wa kawaida, mtoto kuvuja damu ndani kwa ndani, kupatwa na shock, hatari ya ganzi (anesthesia risk) kwa anayefanyiwa upasuaji, na moyo kushindwa kufanya kazi.
  • Madhara kwa mama baada ya kujifungua: maambukizi baada ya kujifungua, kizazi kushindwa kurudi katika hali ya kawaida au damu kuganda kwenye mishipa.
  • Madhara kwa mimba na mtoto atakayezaliwa: Madhara ni pamoja na mtoto kuzaliwa njiti, mtoto kuzaliwa na uzito mdogo, mtoto kuwa na score ndogo (poor Apgar score), mtoto kuzaliwa akiwa amechoka (fetal distress), na upungufu wa damu kwa mtoto
Watoto wanaozaliwa wakiwa na upungufu wa damu hukua kwa tabu, huwa na maendeleo duni ya kiakili na kimatendo (poorer intellectual developmental milestones), uwezekano mkubwa wa kuwa na kasoro mwilini na hata kifo. Kasoro hizo ni pamoja na matatizo ya magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nayo (congenital heart diseases

Dalili
Mjamzito mwenye upungufu wa damu wa kawaida mara nyingi anaweza asioneshe dalili zozote. Hata hivyo iwapo upungufu ni mkubwa, dalili za awali ni pamoja na uchovu wa mara kwa mara na kupumua kwa shida, kukosa hamu ya kula, mapigo ya moyo kwenda kasi, na kuchafuka kwa tumbo.
Wakati wa uchunguzi mjamzito anaweza kuonekana mweupe kuliko kawaida hasa sehemu za viganjani, kucha za vidoleni, ulimi, au macho. Anaweza pia kuwa na dalili za kuvimba miguu.

Vipimo na uchunguzi
Uchunguzi wa upungufu wa damu hufanywa kuwa kupima kiasi cha haemoglobin pamoja kufanya kipimo kingine cha damu kijulikanacho kama peripheral smear.
Vipimo vingine vya maabara ni pamoja na kipimo cha kufahamu uwezo wa kuhifadhi madini ya chuma yaani total iron binding capacity (TIBC), kiasi cha feritin katika damu, kiasi cha folic acid. Katika mazingira mengine kipimo cha kuchukua sehemu ya supu ya mifupa na kuichunguza maabara yaani bone marrow biopsy kinaweza kufanywa. Hata hivyo hivi si vipimo vinavyofanywa mara kwa mara.

Matibabu
Mama mjamzito huitaji miligramu 2 mpaka 4.8 za madini ya chuma kila siku. Ili aweze kupata kiasi hiki, inampasa kula kati ya miligramu 20 mpaka 48 za madini ya chuma. Kwa jamii ambayo upatikanaji wa vyakula vyenye madini hayo ni wa shida, suala hili linaweza kuwa gumu sana kutekelezeka, ndiyo maana Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imeweka mpango maalum wa kuwapa wajawazito wanaohudhuria kliniki madini ya chuma na folic acid ili kufidia pengo hilo.
Vidonge vya madini ya chuma ni salama, nafuu na njia makini ya kuongeza na kurekebisha upungufu wa damu mwilini. Kwa wajawazito ambao hawawezi kunywa, kwa sababu yeyote ile, njia ya sindano inaweza pia kutumika.
Wajawazito wanashauriwa kutumia miligramu 60 za madini ya chuma (ferrous sulphate) na 500mg za folic acid kila siku, ambapo utaratibu huu huendelea kwa miezi mitatu mpaka sita ili kuongeza hifadhi ya madini ya chuma mwilini, hata kama kiwango kinachotakiwa kitakuwa kimefikiwa.

Utumiaji wa vidonge vya madini ya chuma na baadhi ya vyakula: Kuna baadhi ya vyakula kama vile chai ya rangi ambavyo vikiliwa wakati mjamzito amekunywa vidonge vya madini ya chuma vinaweza kupunguza unyonyaji wake katika utumbo. Kwa upande mwingine baadhi ya vyakula vyenye vitamini C kama vile matunda ya jamii ya machungwa huongeza uwezo wa utumbo kunyonya madini ya chuma mwilini.

Vyakula vya kuongeza damu: Pamoja na mkakati huo, wajawazito hushauriwa pia kula vyakula vyenye madini ya chuma kwa wingi kama vile nyama, maini, mayai, samaki, mimea jamii ya kunde, maharage makavu, mboga za majani, matembele, na mikate iliyoongezwa madini ya chuma.

Matibabu ya upungufu wa damu mkali kwa wajawazito walio katika wiki za mwisho (baada ya wiki ya 32): Wagonjwa wa kundi hili hutibiwa hospitali. Wengi wanaweza pia kuwa na dalili za matatizo ya moyo, hivyo wanapaswa kulazwa na kupumzika kitandani, na wakati fulani kuongezewa hewa ya oksijeni. Pamoja na kutibiwa matatizo ya moyo, huongezewa pia damu (packed red cells) kwa vile vidonge vya madini ya chuma havitafaa kurekebisha tatizo hili kwa haraka kabla ya muda wa kujifungua kufika.

Matibabu ya maradhi mengine: kwa mazingira yetu, magonjwa kama malaria na minyoo huchangia kwa kiasi kikubwa kutokea kwa upungufu wa damu kwa wajawazito, hivyo basi magonjwa haya hayana budi kutibiwa kikamilifu ili yasilete madhara kwa mjamzito. Wajawazito wanaoishi maeneo yenye malaria kwa wingi hupewa dawa za SP kwa ajili ya kuwalinda wasipatwe na ugonjwa huu. Pia dawa za minyoo za Albendazole au mebendazole hutolewa kwa wajawazito baada ya miezi mitatu ya mwanzo ili kuua minyoo. Ili kuzuia kujiridia kwa minyoo, wajawazito pia hushauriwa kuvaa viatu/kandambili kila wakati, na kuhakikisha miili na mazingira yao yapo safi.

Dalili na Ishara za Ujauzito

Mstari wima mweusi hutokea tumboni kuanzia chini ya kitovu

Dalili za ujauzito hutofautiana kati ya mwanamke na mwanamke, ingawa kuchelewa au kukosa hedhi ni dalili moja muhimu sana

Ni muhimu kuzitambua na kuzifahamu dalili hizi kwa sababu zinaweza kusaidia kuelezea au kutofautisha matatizo mengine mbali ya ujauzito.

Hebu sasa tuangalie dalili na ishara za Ujauzito:

  • Kutokwa damu kidogo ukeni wakati kiumbe kikipandikizwa kwenye mfuko wa uzazi, ingawa siyo wanawake wote hupatwa na dalili hii
  • Kukosa hedhi, hii ni moja ya dalili kubwa za ujauzito
  • Maumivu ya matiti na kuvimba matiti (huweza kutokea kati ya wiki ya 1 hadi ya 2)
  • Uchovu, wanawake wengi hujihisi uchovu na hali ya kutopenda kufanya lolote.
  • Kupoteza ladha au kuhisi ladha ya chuma mdomoni
  • Kuongezeka kwa hisia ya harufu, kipindi cha ujauzito wanawake wengi huongezeka hisia ya harufu
  • Kichefuchefu na kutapika
  • Maumivu ya kichwa
  • Kizunguzungu
  • Kukojoa mara kwa mara (hasa kati ya wiki 6-8)
  • Kubadilika rangi kwa ngozi inayozunguka chuchu kuwa nyeusi
  • Kutamani baadhi ya vyakula na kuchukia vingine
  • Kupanuka kwa mfuko wa uzazi
  • Tumbo kujaa au kuvimbiwa
  • Kununa na kukasirika haraka
  • Kiungulila au kupata choo kigumu
  • Kolostramu kuanza kutoka kwenye matiti
  • Kuongezeka uzito
  • Kuweza kupapasa mtoto (palpation of the baby)
  • Kulainika na kuvimba kwa shingo ya uzazi (Hegars sign) - kuanzia wiki ya 6
  • Shingo ya uzazi kubadilika rangi kuwa ya samawati kutokana na msongamano wa damu katika mishipa ya vena. Ishara hii huitwa pia Chadwick's sign

Dalili nyingine ni pamoja na

  • Mstari wima mweusi hutokea tumboni kuanzia chini ya kitovu (linea nigra)
  • Mama kuhisi mtoto akicheza (kuanzia wiki ya 20)
  • Maumivu ya mgongo hasa mimba ikishakuwa kubwa.
  • Kipimo cha mimba kuwa chanya (positive).
  • Kusikia mapigo ya moyo ya mtoto
  • Mtoto kuonekana kwenye kipimo cha ultrasound

Seli Asilia Kuongeza Uwezo wa Kushika Mimba kwa Wanawake(Can Stem Cells Increase Women Fertility?)

mja mzito

Wanasayansi wamegundua seli asilia (Stem Cells) kwenye mayai ya mwanamke (Ovaries) ambazo baadae zinaweza kutengeneza kiwango kikubwa kisicho na ukomo cha mayai ya uzazi ya awali (Oocytes).

Kwa kawaida mwanamke huwa na mayai mengi ya uzazi ya awali (Oocytes) wakati akiwa kwenye tumbo la mamake yaani bado akiwa kijusi (Fetus) ambapo anakadiriwa kuwa na mayai milioni 7, na mayai hayo kupungua hadi kuwa milioni 1 wakati anazaliwa na kufikia mayai 300,000 wakati wa kuvunja ungo au kubaleghe. Mayai haya huisha kabisa akifika umri wa miaka 40 hadi miaka ya mwanzoni ya 50 (yaani kipindi cha ukomo wa kupata hedhi), na hii ndio huchangia mwanamke kutokuwa na uwezo tena wa kushika mimba ambao ni tofauti na wanaume ambao bado wanakuwa na uwezo wa kutoa shahawa hata wakiwa wazee.
Utafiti huo uliofanywa na wanasayansi katika hospitali ya Massacheutts nchini Marekani ambapo wanasayansi hao waliweza kuzitenganisha seli hizo kwenye maabara na kutengeneza mayai ambayo wamesema yanauwezo wa kurutubishwa (fertilized) na kuwa mimba.
Kutokana na utafiti huu, wataalamu wengi wa afya wamesema matokeo ya utafiti huu yatabadilisha kabisa tiba ya ugumba kwa wale wanawake wasioweza kushika mimba na pia yanaweza kusaidia wanawake kuwa na uwezo wa kushika mimba kwa muda mrefu zaidi kuliko ilivyo hivi sasa.
Ugunduzi huu ni changamoto kubwa wa dhana ya kwamba wanawake wana kiwango maalum cha mayai ambacho kikishaisha hawawezi tena kutoa mengine na hivyo kukosa uwezo wa kushika mimba tena.
Mayai hayo yaliyozalishwa maabara yalikuwa ya kawaida na hata yalipopandikizwa kwenye tishu ya mayai ya uzazi ya kawaida ya binadamu (Living human ovarian tissue) ambapo hapa walitumia panya, yalikuwa kama kawaida kwa muda wa wiki mbili. Ikumbukwe ya kwamba tafiti nyingi za mambo ya uzazi hufanywa kwenye panya kutokana na kuwa na maumbile ya uzazi yanayoshahabiana na ya binadamu.
Dk Jonathan Tilly ambaye aliongoza utafiti huu amesema ‘’Matokeo ya utafiti huu yamefungua milango mipya katika tekinolojia ya tiba ya ugumba kwa wanawake na pengine pia yanaweza kutumika kuchelewesha kushindwa kufanya kazi kwa mayai ya mwanamke (Delay timing of ovarian failure)’’.
“Hizi seli za asilia, zikiwekwa nje ya mwili wa binadamu zinafurahia kuzalisha mayai mapya zenyewe na kama tutaweza kuongoza hatua hii basi kuna uwezekano hapo baadae tukawa na uwezo wa kuzalisha mayai mengi ya uzazi ya binadamu bila ukomo wowote ule” Mwisho wa nukuu.
Timu yake iliweza kugundua seli hizi za asilia wakati wakitafuta protini maalum ya aina ya DDX4, inayopatika mahsusi katika seli za mayai ya mwanamke.
Kutokana na sababu za kisheria, wanasayansi hao hawawezi kutumia seli hizi kutengeneza kiinitete cha mwanadamu (Embryo). Lakini seli aina hizo hizo zilichukuliwa kutoka kwenye panya zimeweza kutumiwa kutengeneza kiinitete cha panya katika utafiti ulichapishwa katika jarida la Nature Medicine Journal.
Vitengo vingi vya kusaidia kutungisha mimba nje ya kizazi (In Vitro Fertilisation) vinakuwa na mayai ya uzazi machache sana yaliochangiwa na wanawake au vina uwezo mdogo sana wa kuchuma mayai kutoka kwa wanawake.
Wengi wa wanawake katika nchi zilizoendelea wamekuwa wakitoa mayai yao na kuhifadhiwa katika barafu (Frozen eggs) ili waweze kuendelea na mipango yao ya masomo na kazi mpaka hapo baadae watakapo kuwa tayari basi waweze kutimiza ndoto yao ya kuweza kushika mimba na hivyo kupata mtoto.

Tuesday, March 31, 2009

Nina mimba ya miezi 8, salama kungonoka

Nina mimba ya miezi 8, salama kungonoka?


"Mie ni msichana wa umri wa miaka 23,nimepata ujauzito wa rafiki yangu wa kiume wa miaka takribani 5, tulianza kufanya mapenzi mwaka jana tu yani baada ya miaka minne ya uhusiano wetu sasa maswali niliyonayo ni haya:kwanza sijafanikiwa kuskia utamu wa ku-come nikitombwa mie huskia kama nililambwa kisimi
tu ntaanzaje kuskia hivo?

Nimefanya mapenzi mara tatu tu! ya tatu ndo nimepata ujauzito na sijafanya tena kwakuwa boyfriend alikuwa kikazi marekani ila anarudi jumatatu hii na tutafanya mapenzi.

Nina mimba ya miezi 8, je is it safe kufanya mapenzi? na style gani zitamchengua?nikivaa shanga je ntachemsha na mtumbo wangu?Nipo freshi kiafya sina matatizo ya ujauzito...nashukuru ...".

Jibu: Awww umeshika mimba kabla hujautambua na kuujua mwili wako vizuri, kwanini hukutumia Condom? Usijali wala kujisikia vibaya kwani hatuwezi kubadili kilichotokea lakini naamini kabisa mara tu baada ya kujifungua na Mpenzi wako akiwa karibu utafanikiwa kuujua utamu wa kufanya mapenzi/ngono.

Kwa kuanzia mpenzi wako akija mwambie akupe ngono ya mdomo (akushukie chini) na kucheza na kisimi hakika utapata utamu wa ngono ukoje.......

Ikiwa Dakitari au Mkunga wako hajasema kama una matatizo yeyote basi utakuwa salama kabisa kufanya mapenzi japokuwa unapaswa kuwa mwangalifu usije ukakorofisha au kushitua mambo mengine kabla ya wakati. Miezi nane ni mingi au niseme tumbo ni kubwa sana na hata wewe mwenyewe utakuwa umejichokea kiaina hivyo mikao utakayohitaji kufanya mapenzi ni ile ya ku-relax zaidi kama "spoony".

Ambapo baada ya kuandaliwa unalalia ubavu (natumaini ndivyo unavyolala kutokana na ukubwa wa tumbo) kisha yeye mpenzi wako analala kwa nyuma,kisha wewe unapanua mguu ili aweze kuingiza uume kisha rudisha mguu juu ya mguu mwingine (kama ulivyokuwa) na yeye anaendelea kukufanya taratibu mpaka wote mtakaporidhika au maliza haja zenu.

Vilevile mnaweza mkafanya kifo cha mende wewe ukiwa juu (kama umekaa vile) na hakikisha anakupeleka taratibu ikiwa huwezi ku-ride au kifo cha mende wewe juu lakini mpe mgongo (inaitwa doggie lakini sio hatari kama ile ya kuinama/bong'oa) nautazame miguu yake.

Kamwe usifanye mikao au mitindo mingine kama "doggie" zaidi ya hii mitatu.

Ngono baada ya kujifungua

Jinsi ya Kungonoana kwenye Ujauzito