Tuesday, March 17, 2009

Ngono Salama

Ngono Salama

Kila mmoja wetu anahusika kwa namna moja au nyingine kuhusiana na swala la UKIMWI (unavirusi, unaugua, ndugu, jirani, rafiki na jamaa wamekufa via HIV).

Utafiti unaonyesha kuwa kila mwananchi anajua nini maana ya gonjwa hili, jinsi ya kujikinga, kuepuka na kuishi na mtu mwenye virusi na anaumwa na yule mwenye virusi lakini hajaanza kuumwa.


(1)-Watu wengi hawatambui nini maana ya kufanya Ngono salama, wengi wanadhani kutumia mipira(Condoms) ndio Ngono Salama.


Matangazo mengi kupitia vyombo vya Habari husisitiza kufanya ngono salama lakini hawaelezi wazi ni vipi mtu atajua kuwa alifanya/anafanya/afanye Ngono Salama


(2)-Kutokulielewa vema swala zima la ngono, kwamba ili kuifurahia ngono sio lazima uifanye na watu wengi tofauti bali unaweza ukafanya yote utakayo na mpenzi wako huyo uliyenae……..swala muhimu ni mawasiliano na uwazi wa kile unachokitaka kutoka kwa mwanamke/mwanaume.


(4)-Kutokuelewa vema tofauti za maumbile yetu hasa pale tunapoambiwa mwanamke huambukizwa/ambukiza kirahisi kutokana na maumbile yake…..ikimaanisha kutokana na uke ulivyo basi mwanamke yuko hatarini zaidi kuliko mwanaume.

Sasa kwa vile haliwekwi wazi, baadhi ya watu wanadhani kwa vile uke ni mwekundu au pinki basi ni kama jeraha kwamba mwanaume mwenye virusi akigusa tu kitu na box…..la hasha,
.........nadhani inamaana kuwa uke ni rahisi kuchubuka/kwaruzika hasa kama unatumia bidhaa za kufanya uke unukie kimanukato,

Vitu Vinavyochubua Uke

-Kufanya mapenzi ukiwa hauko tayari

-Kuishiwa hamu ya kufanya mapenzi katikati yakufanya mapenzi na kusababisha ukavu ukeni.

-Kujisafisha na kuruhusu sabuni kuingia ukeni,

-Utumiaji wa vifaa vya kuzuia damu ya hedhi kama vile tampax n.k.



Ili kupunguza maambukizo na hatimae kutokomeza kabisa “maambukizo mapya” UKIMWI ni vyema basi sote tushirikiane na kuzungumzia swala hili kwa uwazi zaidi, hakuna haja ya kufichaficha, kwani kila mtu anafahamu kuwa kwa asilimia kubwa gonjwa hili linaenea kwa kufanya ngono isiyo salama.

Watu wanapoamua kufanya ngono hawaendi moja kwa moja kukutanisha miili yao, huenda hatua kwa hatua (kuandaana/chezeana) na hatimae kukutanisha miili yao. Lakini je! hatua hizo za awali kabla ya kufanya tendo lenyewe ni salama?

Hapana, si salama japokuwa watu hudhani kuwa ni salama.

Vilevile baadhi ya watu wanaamini kuwa kuingiliani kimwili (kukutanisha Uume na Uke) ndio pekee kunakopelekea maambukizo na badala yake huridhika kwa kutumia mikono/kuchezeana/kupigana nyeto kitu ambacho ni kizuri lakini je unaposhika nyeti ya mwenzio unauhakika vidole/mikono yako na nyeti zenu hazina mikwaruzo?

Hapa pia tunaona kuwa hata hand job sio salama japo it sounds salama.


JE UTATAMBUA VIPI KUWA ULIFANYA/UNAFANYA NGONO SALAMA?

-Kushikanashikana sehemu mbalimbali za mwili kunaweza kupelekea maambukizo ya Ukimwi, Mfano mwanaume anapopeleka vidole vyake kwenye uke na kugusa majimaji(Vaginal Fluid) alafu baadaye akagusa Uume wake ili kuvaa Kondom ni moja kwa moja yuko kwenye hatari ya kupata virusi vya Ukimwi.


-Mwanamke pia yuko hatarini ikiwa atagusa Manii (Semen) kwa mikono yake na kisha kujishika/kujigusa kwenye Uke wake. Mwanamke pia atakuwa kwenye hatari ikiwa ameondoa nywele sehemu nyeti kwa mtindo huu kunyofoa (pluck Brazilian style) ambao huacha vijitudu vilivyo wazi ambavyo vitapelekea Manii kupenya na kusababisha maambukizo.


-Kupena mapusu ya mate, tafuta mtindo tofauti wa kubusu ili usipate mate kwani huwezi jua kama mpenzi anamikwaruzo kooni au sehemu yoyote ndani ya mdomo wake.


JIKINGE

-Kondom ivaliwe haraka sana baada ya kuvua nguo ya ndani, haijalishi kama utafanya ngono au la!. Pia hakikisha huingizi ulimi wako ndani sana ya mdomo wake na hakikisha hupati kabisa mate kutoka kinywani kwake……tafuta njia mbadala ya kuibua nyege zake kuliko kubusu kwa mate.

-“Withdrawal” (kukojolea nje) baadhi ya watu wanaamini kuwa kufanya hivyo huepusha mimba zisizotarajiwa na maambukizo ya Ukimwi(wakidhani kuwa ni manii pekee ndio hubeba virusi), lakini ifahamike kuwa jinsi tendo linavyoendelea kabla (mwanaume) kufikia kileleni na “kuwithdrawal”ndivyo Manii yanavyobaki ndani ya Uke na kujikuta umeambukizwa bila wewe kujijua.

-kamwe usikubari kufanya ngono bila kinga (skinny dipping) hata kidogo, wakati wote angalia kuwa Kondom inayotumika haina mipasuko n.k.

-“Going Down” wataalam wa magojwa ya zinaa wanakili kuwa mtindo huu wa kutumia mdomo si hatari sana ikiwa tu, hakutakuwa na michubuko nje/ndani ya mdomo, matatizo ya koo, kuvuja damu kwa fidhi n.k.

-Kamwe usijaribu kufanya hivi wakati ukijua kwa unamatatizo ya fidhi, koo, ulimi n.k, lakini ni vyema ikafahamika kuwa ni vigumu sana kugundua kuwa unamichubuko kwenye mdomo, ulimi na hasa koo.

No comments:

Post a Comment