Tuesday, March 24, 2009

Ndoa na Kuzaa

Ndoa na Kuzaa


Swala la kuzaa kwa wanandoa ni uamuzi wao wenyewe kwani wao ndio watakao kabiliana na malezi ya mtoto/watoto wao, mwanamke aliyeolewa ndie atakae kabiliana na mabadiliko na misuko-suko inayohusiana na swala zima la kuzaa na hakuna hata mtu mmoja kati ya wale wanaolalamika kuwa "ndoa" fulani haina mtoto toka ifungwe atakae kuja kusaidia.


Hivyo ni vyema jamii ya kibongo hasa wanawake kuondoa kasumba kuwa as soon as ukifunga ndoa basi kinachofuata ni mtoto. Swala la kuzaa ni uamuzi wa wanandoa husika wawili "kumimbana" na kupata mtoto.

Unapozaa mtoto unafanya hivyo kwa sababu ninyi wawili mmekubaliana na sio kwa vile jamii inayokuzunguuka inataka mfanye hivyo.

Ukileta swala la vitabu vya dini vinasema "tufunge ndoa na tuzaliane tuijaze dunia" hakikisha unafuata kila jambo lililoandikwa kwenye vitabu hivyo vitakatifu......vinginevyo waache wanandoa waishi maisha yao kwa kufuata mipango yao kwani maisha ni kujipangia!

Hii kitu sio Utamaduni bali ni kasumba ya kipuuzi ambayo haina tofauti sana na ile kuwa mke hapaswi kufurahia tendo la ndoa bali mumewe.

No comments:

Post a Comment