Showing posts with label Misingi ya Uhusiana wa Kimapenzi. Show all posts
Showing posts with label Misingi ya Uhusiana wa Kimapenzi. Show all posts

Tuesday, March 31, 2009

Jiandae unapoelekea kwenye uhusiano

Jiandae unapoelekea kwenye uhusiano




Kuna swala la wanawake kudhani kuwa "ndio imetoka hiyo" yaani ndio milele, mara tu anapoanzisha uhusiano na mwanaume……..

na kwa bahati mbaya wengi huishia “disappointment” na kuwaita wanaume wa kibongo hawana mapenzi ya kweli…….sio hawana mapenzi ya kweli bali wewe ndio ulikuwa na haraka au nyote wawili mlikuwa na haraka na hamjui nini maana halisi ya neno “mapenzi”.


Siku hizi vijana tuna haraka sana ya kufanya mambo ambayo hufanywa kwenye committed relationships sasa sijui ni maendeleo au ni wanaume kutokuwa wazi pale wanapotaka kuwa na uhusiano fulani na mwanamke?


Napenda utambue kuwa kukutana na mwanaume/mwanamke na kuwa nae na kupeana miili yenu haina maana huyo ni uhusiano tayari, uhusiano hujengeka baada ya kutoka na huyo mtu kwa muda fulani minimum miezi kama 3 hivi au zaidi……

Hata kama alikujia na gia ya “nataka uwe mpenzi wangu”…..huwezi ukawa mpenzi ktk siku chache……unahitaji muda kuwa na uhakika na hisia zako.


Unajua zamani watu walipokuwa wakikutana, walikuwa hawakimbilii kungonoana, walikuwa wanaheshimiana na kama ni kukutana basi inakuwa mahali peupe kuepusha vishawishi vya kungonoana na hali hiyo iliwawezesha kuvuta muda na kuwa na uhakika na hisia zao kuwa kweli wanapendana.


Na ndio maana wakati huo walikuwa wakiamini (jua) kuwa mwanaume akikupenda kweli basi atavumilia na atakuja kuwaona wazazi na kufunga ndoa na wewe……ndio kungonoka kunafuata.


Tofauti na sasa ambapo tuna swala la ku-date ambapo penzi huibuka....…kisha tunahamia kwenye Trial (move in together and all) na kuangalia mambo yanavyokwenda….je mnapatana? mnaendana ki-life style, kingono mko sawa n.k.


Alafu ndio penzi la dhati hujengeka vema zaidi kwa vile utakuwa unamjua mwenzio kwa undani na hivyo kufanya uamuzi wa busara kama unaweza kumvumilia na kushi nae maisha yako yote au la.


Natambua kuwa kuna watu wengi (hasa wanawake) wanaendeleza imani kuwa kama mwanaume anakupenda kweli basi atakwenda kujitambulisha kwa wazazi wako na atafunga ndoa na wewe……..


Kutokana na nyakati hizi za mwisho I MEAN SAYANSI YA TEKINOLOJIA a.ka maisha ya kisasa ni wazi kuwa hawajui tofauti ya kupendwa na uamuzi wa kuishi na wewe maisha yake yote na matokeo yake ni disappointment.

Zingatia haya.....

Napenda kukwambia kuwa unapoanza uhusiano na mwanaume chukulia mambo taratibu na usikimbilie kufanya ngono kwani kufanya hivyo automatically kutakufanya udhani kuwa tayari uko kwenye uhusiano,


*Angalia mambo ambayo uta-offer ikiwa utakuwa kwenye uhusiano na sio kutegemea afanye hivi au vile

*Weka 50-50 na sio asilimia mia moja kuwa uhusiano utakuwa kama unavyotaka

*Usitegemee mambo makubwa yafanyike ndani ya uhusiano wako na badala yake acha yatokee yenyewe bila kulazimisha.

*Kuwa wazi na kuyazungumzia yale ambayo ungependa yafanyike ktk maisha yenu ya baadae lakini sio kwa kulazimisha au kununa ikiwa mwenzio anaonyesha kutovutiwa na mazungumzo hayo na badala yake wewe furahia kila siku kama inavyokujia……


* Kumbuka mapenzi ya kweli huchukua muda kujengeka na yakijengeka huwa hayabomoki……hata kama mtaamua kuachana baadae mahaba yataisha lakini penzi siku zote hubaki moyoni.

penzi ni nini hasa

Misingi ya Uhusiana wa Kimapenzi

Mapenzi na Technologia

Kupenda kwa vitendo

Yale yanayoweza kuharibu ndoa!

Tuesday, March 17, 2009

Misingi ya Uhusiana wa Kimapenzi

Misingi ya Uhusiana wa Kimapenzi


Katika uhusiano wowote wa kimapenzi yafuatayo ni muhimu na bila haya hakuna sababu ya kusema "mnapendana" au kuendelea kuishi/kuwa pamoja.

1.Ushirikiano-Mnahitaji nguzo hii katika nyanja zote yaani kiuchumi, kimwili, kiutendaji (kuanzia shughuli za ndani mpaka zile za chuo/shule), kimawazo n.k.

2.Mawasiliano-Wengi huwa tunazungumza/eleza ikiwa tunafurahishwa tu lakini kukiwa na matatizo au mabadiliko ktk uhusiano huwa tunaugulia ndani kwa ndani kitu ambacho si kizuri na kinaweza kuharibu uhusiano wenu. Ni vema kuzungumza wazi na kuhoji kwa upole na upendo ikiwa hufurahishwi na lolote ndani ya uhusiano wako kuanzia utendaji wake kitandani, matumizi ya pesa,wasiwasi n.k. hii itamsaidia kuona tatizo liko wapi na hivyo kushirikiana kulitatua na hivyo kuendeleza penzi lenu.

Heshima-Kutokana na swala la Usawa wa wanawake wengi wamekuwa na viburi. Pamoja na Elimu yako ya juu na mshahara wako mkubwa kuliko yeye heshima inatakiwa kwenye uhusiano wenu ili uwe wenye afya na wa muda mrefu, heshima haishii hapo bali ni kutotoka nje ya uhusiano wenu, kutojiachia na kuonyesha tabia mbovu kama vile kulewa kupita kiasi, kuongea non stop, kuzungumzia maswala ya chumbani, maumbile yake au utendaji wake mbele za rafiki na ndugu zake bila kusahau kukaribisha “shemeji marafiki” nyumbani bila yeye kuwa na taarifa na mwisho kabisa kufanya maamuzi makubwa bila kumuhusisha mwenzio.

Masikilizano na maelewano/makubaliano-Jifunze kusikiliza na kuelewa pale mnapozungumza, si unajua kuna zile “ups na downs seasons”? Kwamba kuna wakati mnafarakana kiaina ndani ya uhusiano na mmoja wenu anasusa/haongei na wewe.

Wanawake wengi wana tabia ya kutolianzisha na akianza basi ni kuingilia mazungumzo kwa vile tu kilichosema kimewagusa (ukweli au uongo) lakini kwa kufanya hivyo hakuna mtu atakaemuelewa mwenzie, hata kama jambo lilikuwa la kawaida tu na kuhakikishia mtaishia kubishana na msifikie muafaka.

Sisemi kuwa ubaki kimya na kuwa “ndio bwana” bali najaribu kusema kuwa ni vema kujifunza kusikiliza na kuelewa kwanza kabla hamjakubaliana na kufikia muafaka kuhusu swala husika.

Kujali-Sote huwa tunaonyesha kujali ikiwa wenza wetu ni wagonjwa, lakini wengi huwa tunajisahau mara baada ya kuwekwa ndani iwe ni kisheria, kidini au kisasa(wengi huwa tunaita trial unapima kama mna-get on well b4 ndoa raha tupu ila huruhusiwi kuzaa shaurilo).

Wanawake wengi wana tabia ya kujali watoto wao,marafiki zaidi ya wenza wetu. Vilevile siku hizi kuna hii tekinolojia basi watu twashinda simuni au komputani kuzungumza na marafiki badala ya wapenzi wetu kitu ambacho huwaumiza sana hawa viumbe kihisia lakini kwa vile wameumbwa kuficha hisia zao huwezi kujua, sana sana atachoropoka nje bila wewe kutambua.

Kujali hisia za mwenzako ni muhimu, hivyo kama kuna kitu kinakutatiza au kinakufanya wewe ushindwe kuonyesha hali yakujali kwa mpenzi wako basi rudi kwenye kipengele cha mawasiliano.