Saturday, December 24, 2011
Utafiti Unaonyesha Kwamba Wanawake Hubakwa na Waume Zao
Tafiti zilizofanywa na wataalama wa masuala ya afya na jamii zinadai kuwa baadhi ya wanawake waliomo katika ndoa hukumbana na kadhia ya kubakwa na wanaume zao na pia hudhalilishwa. Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali ambalo hujishughulisha na Afya na Maendeleo ya Mtoto-(KIWOHEDE), Justa Mwaituka amesema kuwa wanawake wengi walio kwenye ndoa wananyanyaswa na waume zao kwakuwa wanalazimishwa kufanya mapenzi kinyume na maumbile pamoja na kufanya kwa njia ya mdomo.
"Iringa tumekutana na wanawake ambao wamezikimbia ndoa zao kutokana na kuingiliwa kinyume na waume zao pamoja na kulazimishwa kufanya ngono kwa njia ya MDOMO"anasema Mwaituka.
Source Mwananchi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment